Mapigano kati ya vikosi vya Uganda na DRC katika ziwa Edward

Kumeshuhudiwa visa kadhaa kati ya vikosi vilivyojihami Congo na vikosi wa Uganda. Haki miliki ya picha AFP
Image caption Kumeshuhudiwa visa kadhaa kati ya vikosi vilivyojihami Congo na vikosi wa Uganda.

Watu 7 wamefariki wakiwemo wanajeshi 4 wa Uganda katika mapigano kwenye ziwa Edward kati ya vikosi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo na Uganda, kwa mujibu wa afisa wa Congo aliyenukuliwa na shirika la habari la AFP.

Ziwa Edward lipo katika mpaka kati ya nchi hizo mbili.

Kiongozi kutoka Beni, Donat Kibwana, amenukuliwa na AFP akisema kuwa mashua ya kupiga doria ya Congo ilishambuliwa Alhamisi asubuhi na boti la kupiga 'doria la Uganda'.

Boti la Uganda lilizama na wanajeshi wanne wa taifa hilo na raia watatu walifariki, aliongeza.

Twaweza: Watanzania 'hawako tayari kuandamana'

Onyo la Macron kuhusu vituo vya wahamiaji Afrika

Jaribu Muliwavyo, mbunge kutoka eneo hilo, amekiambia kituo kimoja cha redio Congo kwamba mapigano hayo yanatokana na mzozo wa haki za kuvua.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Afisa kutoka Beni DRc amesema mapigano hayo yanatokana na mzozo kuhusu haki za kuvua

Msemaji wa jeshi la Uganda, Brigedia Richard Karemire, amewashutumu "wanaume waliojihami waliorusha guruneti ndani ya boti letu la kupiga doria", linaripoti gazeti la New Vision Uganda.

Shambulio hili limetokea katika mto huo upande wa Congo katka jimbo la Kivu kaskazini.

Sio mara ya kwanza ghasia kushuhudiwa kati ya Uganda na DRC

Mwandishi wa BBC anaeleza kuwa kumeshuhudiwa visa kadhaa kati ya vikosi vilivyojihami Congo na vikosi wa Uganda.

Mama mwenye miaka 91 amuua mwanaye kuepuka kwenda nyumba ya kulea wazee

Wanausalama wa Ethiopia tuhumani

Mwezi uliopita, Uganda iliwakamata kwa muda wavuvi 48 kutoka DRC ikiwashutumu kwa kuvuka mpaka wa baharini na kuingia upande wa Uganda.

Katika shambulio jingine tofuati wiki hiii katika eneo hilo la Kivu kaskazini, wanajeshi 8 wanaripotiwa kuuawa katika mapigano kati ya vikosi vya Congo , kundi la waamgambo nchini na wanamgambo wa ADF kutoka Uganda.

Wamekuwepo katika katika jimbo hilo lenye utajiri wa rasilmali kwa miaka kadhaa.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii