Waziri wa zamani nchini Pakistani, Nawaz Sharif ahukumiwa miaka 10 gerezani

Nawaz amekana tuhuma dhidi yake Haki miliki ya picha AFP/GETTY IMAGES
Image caption Nawaz amekana tuhuma dhidi yake

Mahakama nchini Pakistani imemhukumu aliyekuwa waziri mkuu wa nchi hiyo Nawaz Sharif kifungo cha miaka 10 gerezani kwa makosa ufisadi unaohusu majengo manne ya kifahari jijini London.

Hatua hiyo imefikiwa na mahakama baada ya kucheleweshwa kwa muda.

Binti yake na mkwewe pia wamekutwa na hatia

Nawaz Sharif,ambaye kwa sasa yuko London alihukumiwa akiwa hayuko mahakamani, na mwenyewe alisema kuwa hukumu hiyo ina mlengo wa kisiasa.

Jaji Mohammad Bashir amemtaka Sharif kutumikia kifungo cha miaka 10 kwa kosa la kumiliki mali yenye gharama kubwa kuliko kipato chake na mwaka mmoja kwa kutotoa ushirikiano na mamlaka inayopambana na vitendo vya rushwa, NAB.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Ulinzi uliimarishwa nje ya mahahakama mjini Islamabad

Binti yake, Maryam Nawazi Sharif amehukumiwa kifungo cha miaka saba kwa kushirikiana na babaye kwenye uhalifu huo na mwaka mmoja kwa kutotoa ushirikiano kwa mamlaka za kiuchunguzi huku mkwewe Nawaz akihukumiwa kifungo cha mwaka mmoja kwa kutotoa ushirikiano.

Sharif na Maryam wametozwa faini ya pauni milioni 8 na pauni milioni mbili.Kwa sasa wote wako jijini London ambapo mke wa Sharif, Kulsoom Nawaz anapata matibabu kutokana na maradhi ya saratani.

Panama Papers zilizovuja mwaka 2015 zilitoa taarifa kuwa watoto kadhaa wa Sharif walikuwa na mahusiano na makampuni yaliyo nje, ambayo yalidaiwa kupitisha fedha kwa ajili ya kununua mali nje ikiwemo majengo ya anasa jijini London

Familia yake, hatahivyo, inasisitiza kuwa wanamilimiliki mali hizo kihalali. Katika sehemu ya hukumu, Mahakama imetaka mali hizo zitaifishwe kwa serikali.

Waandishi wa habari nchini Pakistani walikita kambi nje ya makazi ya Avenfield, ambako familia ilikuwa ikitazama kesi.

Hukumu imetolewa wiki chache kabla ya uchaguzi mkuu wa Pakisani utakaofanyika tarehe 25 mwezi Julai.Sharifu amepoteza uhalali wa kukiwakilisha chama chake cha PML-N

Kaka yake Shahbaz Sharif hivi sasa anakiongoza chama cha PML-N, na anawania katika uchaguzi huo ujao

Amemtetea kaka yake katika mkutano na waandishi wa habari akisema kuwa hukumu hiyo ina ushawishi wa kisiasa.

Mahakama kuamua hatima ya Waziri Mkuu Pakistan

Nawaz Sharif ajiuzulu baada ya uamuzi wa mahakama

Mahakama ya juu ilimvua madaraka Nawaz Sharif mwezi Julai mwaka 2017 baada ya taarifa ya Panama papers

Shariff alikuwa madarakani tangu mwezi Novemba mwaka 1990 mpaka julai mwaka 1993 na kuanzia Februari mwaka 1997 mpaka alipoangushwa mwezi Oktoba mwaka 1999.