Vijana wa Kenya waliozuru Urusi kutazama kombe la Dunia wazungumza

Vijana wa Kenya waliozuru Urusi kutazama kombe la Dunia wazungumza

Kundi moja la vijana kutoka eneo la Marsabit nchini Kenya limewasili kutoka Urusi ambapo lilikuwa limeenda kutazama mechi kati ya Uhispania dhidi ya Urusi. Mpango huo unatokana na shirika moja la kijamii kwa jina HODI ambalo linawashawishi vijana mjini Marsabit kucheza soka kwa lengo la kuleta amani na mshikamo katika kaunti hiyo huku likiwasaidia wasichana wadogo kukwepa ukeketaji . Walituelezea kuhusu ziara hiyo ya Urusi na umuhimu wake.