Wavulana 4 kati ya 12 waliokwama pangoni Thailand waokolewa

Helkopta ya jeshi nchini Thailand inayoaminika kusaidia kubeba vijana waliookolewa Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Helkopta ya jeshi nchini Thailand inayoaminika kusaidia kubeba vijana waliookolewa

Taarifa za hivi punde zilizotolewa na jeshi la majini la Thailand limesema kuwa wavulana wanne kati ya 12 waliokwama pangoni nchini humo wameokolewa.

Picha zinazoonyesha Helkopta za jeshi na magari ya kubebea wagonjwa zimeonekana katika eneo ambalo shughuli za uokoaji zimekuwa zikiendelea.

Kikosi cha waokoaji nchini Thailand kilianzisha operesheni hatari kuwasaidia wavulana 12 na mtu mzima mmoja kutoka pangoni ambako walikuwa wamenasa humo kwa majuma mawili

kikundi hicho kimekwama kwenye pango la Tham Luang, huku wakizungukwa na maji ambayo kina chake kimekuwa kikiongezeka, maafisa walikata shauri kuwa hawatasubiri zaidi.

Haki miliki ya picha AFP/Getty
Image caption Magari ya kubeba wagonjwa

Wataalam wa upigaji mbizi ambao wamekuwa wakiwasaidia wavulana hao, wanaongoza oparesheni hiyo.

Maafisa wamesema kuwa wavulana hao wako tayari na wana nguvu.

Kinachoendelea pangoni

Watu waliokuwa wamejitolea na vyombo vya habari vilikuwa vimepiga kambi kwenye eneo la kuingilia kwenye pango kwa kipindi cha juma moja lililopita.

Lakini asubuhi ya Jumapili, waandishi wa habari waliambiwa waondoke eneo hilo, hatua iliyoashiria kuwa operesheni ya kuwaokoa vijana imekaribia kuanza.

Narongsak Osottanakorn ambaye amekuwa akiongoza operesheni ya uokoaji, alithibitisha baadae kuwa wapiga mbizi 18 wameingia pangoni kuwafuata wavulana waliokwama.

''Wamekuwa wakiangaliwa na Daktari na wako vizuri kimwili na kiakili.wako tayari kutoka''.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Waokoaji wanalazimika kutumia mbinu mbalimbali kuwaokoa wavulana

Lakini kutokana na majira haya ya mvua ambayo yameanza, mafuriko ambayo yalisababisha wavulana wanasema hali itakuwa mbaya siku zijazo

Waokoaji wamekuwa wakiyatoa maji nje ya pango, na gavana amesema kina cha maji yaliyo pangoni ni kidogo kwa sasa

''Hakuna siku nyingine tutakayokuwa tayari kama leo ,'' alisema Bwana Narongsak.''vinginevyo tutapoteza nafasi''.

Watawatoaje nje?

Hii haijathibitishwa, lakini waokoaji watatumia mbinu kadhaa kama kuogelea majini, kutembea,kupanda na kupiga mbizi

Safari yao inawapitisha katika njia nyembamba, na zenye mabonde, ni zoezi lenye changamoto kubwa, Mwandishi wa BBC Jonathan Head anaripoti karibu na pango .

itahusisha safari ya muda mrefu chini ya maji kwa watoto ambao hawakuwahi kutumia vifaa vya upigaji mdizi.Baadhi yao walilazimika kuwa na darasa la masomo ya kuogelea ndani ya pango

Waokoaji wamepanga kuwasogeza mpaka katika eneo moja ambalo litawarahisishia wapigambizi kuwatoa nje.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Katika Kanisa ,mjini, Chiang Rai watu wameitumia jumapili kuwaombea vijana hao

Mtazamo wa wataalamu kuhusu hatari iliyo mbele

Itakuwa rahisi kwao kutokea eneo hilo mpaka kuufikia mlango wa kutokea pangoni kisha kuelekea hospitali.

Haijajulikana kama watatolewa wote kwa wakati mmoja au kwa makundi.

Kiashiria kuhusu kuwepo kwa hali ya hatari kwenye safari hiyo, mpigambizi wa zamani wa Thailand alipoteza maiha kwenye mapango juma lililopita. Saman Gunan alikuwa amerejea kutoka kwenye shughuli ya kuwapa matangi ya hewa safi.

Alipoteza fahamu na hakuweza kurejea katika hali yake.Wafanyakazi wenzie wamesema ''hatutaacha moyo wa rafiki yetu wa kujitoa kupotea''.

Kwa Picha: Mlipuko wa volkano 'wameza' nyumba za watu Marekani

Waliingiaje kwenye pango na kuna hali gani humo?

Wavulana hao walikuwa sehemu ya timu ya mpira wa miguu ya 'Wild Boars''.wenye umri wa miaka 11 na 16.

Inadhaniwa kuwa walikuwa hapo tarehe 12 mwezi Juni ikiwa ni sehemu tu ya kujumuika kusheherekea siku ya kuzaliwa.

Walijikuta katika mazingira hayo mabaya kwao bila kutarajia.

Hatimaye juma lilillopita, walikua na njaa na wenye hofu.Tangu wakati huo wamekuwa wakipata msaada wa wapiga mbizi ambao wamekuwa wote, wakipata huduma ya maji , chakula mwanga na huduma za kiafya.

Waliweza pia kutuma barua kwenda kwa wazazi wao wakiwaambia wasiwe na wasiwasi, na kuwa watarejea nyumbani.