Serikali ya Uturuki yawafukuza kazi wafanyakazi 18,000

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan

Uturuki imewafukuza kazi wafanyakazi 18,000 wa idara za serikali,hatua inayotokana na jaribio lililoshindwa la kupindua serikali miaka miwili iliyopita.

waliofukuzwa ni wanajeshi,polisi na Aademics, chaneli ya Televisheni na magazeti matatu pia vilifungwa

tangu kutokea jaribio la kuipindua serikali, Serikali imewafuta kazi zaidi ya watu 125,000 na kutangaza sheria ya hatari , kudhibiti vyombo vya habari na upinzani

Hatua hii imekuja wakati Rais Recep Tayyip Erdogan anajianda kuapishwa siku ya Jumatatu.

Erdogan ameahidi kuondoa hali ya tahadhari .Vyombo vya habari vinasema kuwa hatua ya Jumapili huenda ikawa ya mwisho kabla ya siku ya kuapishwa

Rais Erdogan alichaguliwa tena kwa ushindi wa asilimia 53 ya kura, pamoja na kusimamia kuimarisha uchumi amenyooshewa kidole kwa kile kilichodaiwa kukandamiza haki ya kutoa maoni, kudhibiti upinzani na kuwatupa gerezani wapinzani takribani 160,000.

Erdogan ashinda muhula wa pili wa urais Uturuki

Chini ya mabadiliko ya katiba ambayo yaliridhiwa baada ya kura ya maoni ya mwaka jana, Bunge limekuwa likidhoofishwa huku nafasi ya Waziri mkuu ikifutwa

Rais atakuwa na mamlaka ya kuteua mawaziri na makamu wa rais pia kuingilia mfumo wa sheria.

Rais Erdogan amesema mamlaka yake itamsaidia katika kushughulikia changamoto za kiuchumi na kupambana na waasi wa kikurdi kusini mashariki mwa nchi hiyo.