Warembo 16 katika shindano la 'Miss Burundi' wajiondoa

Ange Bernice Ingabire
Image caption Ange Bernice Ingabire (kati kaati) alituzwa Miss Burundi wa mwaka 2016-2017

Wasichana 16 kutoka mikoa ya Burundi waliokuwa wamefika kwenye fainali ya mashindano ya kumteua msichana mrembo Burundi (Miss Burundi) wamejiondoa katika shindalo hilo.

Hatua hiyo sasa inaonekana kutishia uwezekano wa kufanyika shindano hilo kwa mwaka huu 2018.

Wasichana hao katika waraka wao wamesema kuna giza kubwa katika maandalizi ya mwaka huu wakitaja mathalan ahadi za atakachotunukiwa mrembo wa kwanza na wa pili.

Mapema iliahidiwa kuwa mshindi angetunukiwa gari jipya na kupewa kiwanja chenye ukubwa wa mita mraba mia nne.

Lakini pia kuna tuzo la pesa taslim.

Hayo yote wasichana hao wamesema shirika la Burundi Event halija ya andaa.

Shindano hilo la Miss Burundi limedhamiriwa kuonyesha utamaduni, uweledi na urembo wa wanawake wa Burundi.

Huwezi kusikiliza tena
Vijana wa Kenya waliozuru Urusi kutazama kombe la Dunia wazungumza

Fainali hiyo ambayo ilipangwa kufanyika tarehe 21 Julai 2018, ime ahirishwa na shirika la Burundi event limetangaza kuwa fainali hiyo imesukumwa mbele hadi tarehe 28 Julai.

Haijawekwa wazi iwapo shirika hilo lita wateuwa wagombea wapya.

Huenda ikawa ni vigumu kutokana na muda.

Refa wa Kenya apigwa marufuku ya maisha kushiriki kandanda

Njia ya kuutanzua mzozo huu ni kufanya mazungumzo na wasichana hao kukubali kurejea ulingoni.

Lakini pia kabla ya wasichana hawa, wana kamati watano katika shindano hili walijiuzulu.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii