Anisia na Maryness: Pacha walioungana Tanzania wahamishiwa Saudi Arabia kwa upasuaji

Michuzi Haki miliki ya picha MICHUZI BLOG

Pacha wa Tanzania waliozaliwa wakiwa wameungana kifuani hadi miguuni mkoani Kagera mapema mwaka huu wamewasili nchini Saudi Arabia kwa upasuaji wa kuwatenganisha.

Anisia na Maryness Beautus waliwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mfalme Khalid mjini Riyadh wakiandamana na mama yao na kundi la madaktari.

Kisa cha pacha hao kimefananishwa na kisa cha pacha wengine walioungana waliogusa nyoyo za wengi nchini Tanzania Maria na Consolata. Hao hata hivyo hawakutenganishwa na waliishi wakiwa wameungana hadi walipofariki dunia tarehe 2 Juni mwaka huu.

Pacha hao Anisia na Maryness watafanyiwa upasuaji karibuni baada ya Mfalme Salman kutoa idhini ya kufanyika kwa upasuaji huo kwa gharama ya serikali ya Saudia.

Pacha hao walipokelewa na kikosi maalum cha wanajeshi walinzi wa rais na maeneo matakatifu ya Kiislamu katika uwanja wa ndege. Wanajeshi hao walisaidiana na wataalamu kutoka Kituo cha Misaada ya Mfalme Salman (KSRelief) ambao watasimamia matibabu yao na kuchunguza iwapo inawezekana kuwafanyia upasuaji wa kuwatenganisha.

Pacha hao wawili wenye miezi sita wameungana kutoka kwenye koo, tumbo na mfupa wa nyonga. Wana miguu mitatu na kwenye uzazi. Hata hivyo, kila mmoja ana moyo wake.

Wamekuwa wakihudumiwa na madaktari katika hospitali ya taifa ya Muhimbili nchini Tanzania na wamekuwa katika hali nzuri.

Mfalme Salman alitoa agizo la kufanikishwa kwa matibabu ya pacha hao Jumapili ambapo aliagiza pia kwamba Saudi Arabia ilipie gharama yote ya upasuaji huo.

Ujumbe kutoka kwa ubalozi wa Saudia nchini Tanzania ulikuwa umewatembelea pacha hao Muhimbili, Dar es Salaam awali na kupokea taarifa za kimatibabu kuwahusu pacha hao kutoka kwa mkurugenzi wa hospitali hiyo Dkt Lawrence Museru.

Pacha hao wa Tanzania walizaliwa mnamo 29 Januari mwaka huu katika zahanati ya St Thereza Omukajunguti wilayani Misenyi. Walisafirishwa hadi hospitali ya kanda ya Bukoba kabla ya mwishowe kuhamishiwa Muhimbili.

Baba yao Benatus Bernado, 28, alikuwa awali ameambia gazeti la serikali ya Daily News kwamba waikuwa wameshauriwa na madaktari Muhimbili kwamba wataalamu wa Saudi Arabia ndio waliokuwa na uwezo wa kuwatenganisha pacha hao.

"Tunatumai kwamba upasuaji huo utafanikiwa," alisema.

Mama yao pacha hao Jonesia Jovitus ana mtoto mwingine mvulana wa miaka 1.2.

Serikali ya tanzana imekuwa ikifanya mashauriano ya kufanikisha kuhamishiwa kwa pacha hao Tanzania kwa wiki kadha, mazungumzo yaliyomshirikisha balozi wa Saudi Arabia nchini Tanzania Mohammed Bin Mansour Almalik na Waziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania Dkt Augustine Mahiga.

Image caption Pacha Maria na Consolata

Upasuaji wa pacha hao utafanyika katika hospitali maalum ya watoto ya Mfalme Abdullah inayopatikana katika eneo la mkusanyiko wa Hospitali za Mfalme Abdullah zilizoanzishwa Mei 1983. Ndio mkusanyiko mkubwa zaidi wa hospitali ambazo zimo chini ya kitengo cha afya cha kikosi cha wanajeshi walinzi wa rais na maeneo matakatifu mjini Riyadh.

Ni hospitali ambayo imehusika katika kuwatenganisha pacha walioungana awali.

Pacha wa Sudan na Palestina waliotenganishwa

Januari mwaka huu pacha kutoka Palestina Farah na Haneen walitenganishwa na madaktari katika hospitali maalum ya watoto ya Mfalme Abdullah mjini Riyadh ingawa ni mmoja pekee aliyenusurika.

Mshauri mkuu wa kituo KSRelief Dkt Abdullah bin Abdulaziz Al-Rabiah aliyekuwa mkuu wa madaktari waliofanikisha upasuaji huo alisema Farah hakuwa na viungo muhimu vya kumuwezesha kuishi na alikuwa anamtegemea mwenzake. Farah hakuwa na moyo, mapafu na ubongo na haikuwezekana kumuokoa.

Upasuaji wa pacha hao ulichukua karibu saa 15 kumalizika.

Novemba mwaka 2016, wataalamu katika hospitali hiyo waliwatenganisha pacha kutoka Sudan kwa jina Rammah na Waddah katika upasuaji uliodumu saa 11.

Pacha hao walikuwa wameungana kwenye tumbo na mfupa wa nyonga. Walikuwa na miguu mitatiu.

Machi 2016, pacha wengine kutoka Tanzania waliokuwa wameungana kifuani na tumboni walitenganishwa katika hospitali hiyo.

Mwaka 2015, Februari na Machi, waliwatenganisha pacha Abdullah na Abdulaziz kutoka Yemen na mwaka 2009 waliwatenganisha pacha Hassan na Mahmoud wenye umri wa miezi sita kutoka Misri.

Mapacha walioungana wakoje?

Mapacha walioungana huwa ni wachache sana kutokea au kuwepo, katika watoto laki mbili wanaozaliwa kila mwaka anazaliwa mtoto mmoja tu wa aina hiyo.

Watoto wengi huwa hawawezi kuishi ,hufa mara baada ya kuzaliwa au mimba huharibika.

Watoto hawa uzaliwa katika uzao wa yai moja,hufanana na wana jinsia moja.

Kuzaliwa kwa watoto hawa huwa kuna hali ya kustaajabisha,kwa ujumla watoto hao wanaweza kuishi wakizaliwa katika hali hiyo huwa ni kati ya asilimia 5 mpaka asilimia 25.

Katika rikodi za historia zinasema kwamba mapacha wa kuungana wengi wanaoweza kuishi kwa muda mrefu ni wa kike,kwa asilimia 70

Mapacha walioungana wamegawanyika katika sehemu tatu

•73% wameunganika kuanzia kwenye kifua na tumbo

•23% wanakuwa wameunganika katika sehemu ya chini ya mapaja na miguu

•4% wanakuwa wameunganika kichwa

Mapacha walioungana waliowahi kuwa maarufu duniani

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Mapacha Eng na Chang

Kwa miaka mingi mapacha walioungana wameendelea kuishi kutokana na matokeo ya tafiti nyingi zilizofanywa na majaribio mengi ya upasuaji yaliyofanyika

Mapacha wa kwanza wa kuungana waliojipatia umaarufu mkubwa duniani walijulikana kama 'siamese' majina yao yalikuwa ni Eng na Chang .

Mapacha hao walizaliwa mwaka 1811 waliweza kuishi kwa miaka 63 na kufanikiwa kupata watoto 22 kutoka kwa wadada wawili ndugu waliowaoa wakiwa na umri wa miaka 21,Chang alikuwa na watoto 12 na Eng watoto 10.

Walipozaliwa jamii ilitaka kuwauwa lakini kwa kudhaniwa kuwa wataleta mikosi na walioneka kuwa nio viumbe wa ajabu.

Mapacha wa kuungana na maisha yao ya ndoa

Katika karne ya ishirini,mapacha wa kuungana walikuwa wanazuiwa kuoa au kuolewa nchini Marekani

Na hii iliibua hisia za wengi pale ambapo wanamuziki ambao ni wacheza filamu wa nchi hiyo Daisy na Violet walipotaka kuolewa.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Daisy na Violet mapacha waliokuwa wacheza filamu

Watu wengi waliwaona kuwa maumbile yao hayawezi kuwaruhusu kuolewa au kupata wenza ingawa mapacha wenyewe wanajiona wamekamilika.

Kwa upande wa Chang na Eng ambao walifanikiwa kuoa, maisha yao ya ndoa yalikuwa na changamoto nyingi hasa pale ambapo wake zao walipoanza kugombana na kupelekea wake hao kuishi kwenye nyumba mbili tofauti.

Kwa maisha yao yote mapacha hao walikuwa wanaishi kwa mke mmoja siku tatu na mwingine siku tatu.

Vilevile mapacha kutoka Tanzania,Consolata na Maria ndoto yao kubwa baada ya shule ni kuolewa na mume mmoja.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii