Kombe la Dunia 2018: Je uhamiaji umechangia ufanisi wa Ufaransa, Ubelgiji na England?

Kikosi cha Ufaransa kilichocheza dhidi ya Uruguay kwenye robo fainali kilijumuisha wachezaji watano ambao japo mzazi wao mmoja ni mhamiaji : (nyuma, kutoka kushoto): Paul Pogba, Samuel Umtiti; (Mbele) Corentin Tolisso; N'Golo Kante; Kylian Mbappe Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Kikosi cha Ufaransa kilichocheza dhidi ya Uruguay kwenye robo fainali kilijumuisha wachezaji watano ambao japo mzazi wao mmoja ni mhamiaji : (nyuma, kutoka kushoto): Paul Pogba, Samuel Umtiti; (Mbele) Corentin Tolisso; N'Golo Kante; Kylian Mbappe

Timu tatu kati ya nne zilizo ingia nusu fainali ya kombe la dunia zina mambo mbali mbali ya kufanana ukiachana na tofauti zao za kijiografia.

France, Belgium and England timu hizi zote zina idadi kubwa ya wachezaji ambao wazazi wao ni wahamiaji. Sasa tuzungumzie namba:

Wachezaji 16 kati ya 23 wa ufaransa wana angalau mzazi mmoja ambaye amezaliwa nje ya nchi. Wawili walizaliwa katika visiwa vya Carrebean ya Ufaransa ambayo hutajwa kuwa sehemu ya Ufaransa.

Wachezaji kumi na moja wa ubeligiji na saba wa Uingereza ni watoto wa angalau muhamiaji mmoja, na wengine wa nne wa uingereza wana asili ya watu wa africa wanao tokea Caribean. Mmoja wao ni Raheem Sterling aliyezaliwa Jamaica.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Babake Mbappe, Wilfred, ni mhamiaji aliyetoka Cameroon na kwenda Ufaransa

Kikosi cha ufaransa chenye tamaduni mbali mbali si cha kushitukiza.

Timu ambayo ilishinda kombe la Dunia mwaka 1998-Ushindi pekee wa nchi hiyo mpaka sasa-ulisherehekewa kama ishara ya mafanikio ya mwingiliano wa jamii huko ufaransa na timu ilipewa jina la utani la "The Rainbow Team" yaani timu yenye mchanganyiko wa watu kama upinde wa mvua.

Hata hivyo miaka minne baadae kundi hilo hilo lilitishiwa kususiwa na wachezaji wenye asili mchanganyiko katika maandamano kumpinga mgombea anayesimama na siasa kali Jean-Marie Le Pen aliyekuwa akiongoza duru ya kwanza ya uchaguzi wa Rais mwaka 2002 (ingawa alitupwa mbali katika matokeo halisi)

Katika mashindano ya mwaka jana, siasa kali zilirudi tena na mtoto wa Le Pen, Mariane alipata asilimia 33 ya kura ikiwa ni mara mbili ya NFP na kufanana na 2002.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Wachezaji 16 kati 23 katika timu ya Ufaransa ni watoto wa wahamiaji

"Marine Le Pen aliwahi kuweka wazi kuwa akiiangalia Les Bleus (jina la utani la timu ya Ufaransa), 'haitambui ufaransa ama yeye mwenyewe,'" alieleza Afshin Molavi, kutoka chuo kikuu cha masuala ya kimataifa Johns Hopkins kilichopo Washington.

Hakuna tishio lolote la kususia timu kwa sasa, japokuwa katika nusu fainali Ufaransa ndio inakuwa timu inayopendwa na wengi kulibeba kombe la dunia.

Pacha walioungana Tanzania wawasili Saudi Arabia kwa upasuaji

Wavulana wote na kocha wao waliokwama pangoni Thailand waokolewa

Watu 13 wanaoenziwa na Diamond Platinumz

Kikosi cha Ubeligiji kina wachezaji 11 ambao wana angalau mzazi mmoja muhamiaji, ukijumuisha Romelu Lukaku na Vincent Company, ambao baba zao ni wa Kongo. Mfano halisi ni baba yake Lukaku ambaye aliwahi kuichezea timu ya taifa ya Zaire miaka ya 1990.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Timu ya Ubelgiji iliyocheza dhidi ya Brazil, wachezaji 5 wana mzazi japo mmoja aliye mhamiaji: (Nyuma kutoka kushoto) Romelu Lukaku (DRC); Axel Witsel (Martinique); Vincent Kompany (DR Congo); Marouane Fellaini (Morocco); (Mbele): Nacer Chadli (Morocco)

Hii inaleta picha tofauti na timu ya taifa iliyo cheza kombe la Dunia mwaka 2002, kipindi ambacho wachezaji wawili tu wenye asili mchanganyiko walikuwepo katika kikosi hicho.

Kampeni za Urusi zinakuja kipindi ambacho kuna mgawanyiko mkubwa wa wa ki siasa,tamaduni na jamii huko Belgium, nchi ambayo ina mikoa miwili tu na lugha mbili - Wallonia(kifaransa) na Flanders (ki flemish)

Mvutano baina ya makundi hayo mawili ulileta mgawanyiko na muelekeo wa kutaka kujitenga katika uchaguzi wa mwaka 2010 ambapo kilishinda chama cha ki Flemish N-VA hali iliyopelekea nchi hiyo kukaa siku 541 bila kuundwa kwa serikali.

Hata hivyo timu hiyo ina ina wachezaji kutoka mikoa yote miwili na kocha wao ni mu hispania hali inayo onyesha umoja, na hii inasababishwa na ukweli kwamba wachezaji wanao unda kikosi hicho wanafanya biashara zao Uingereza.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Mchezaji wa kiungo cha kati wa Ubelgiji Alex Witsel asherehekea na umati ushindi wa timu hiyo dhidi ya Japan

"Sipo kwenye michuano ya kombe la dunia kuzungumzia siasa. Mashindano haya ni nafasi ya kusherehekea kama nchi mmoja na kuiunga mkono timu inayo inayowakilisha ubeligiji yote.," Mshangiliaji wa Ubeligiji Jan Aertssen ameiambia BBC wakati ambapo timu hiyo ilishinda dhidi ya Brazil.

"Watu ambao wanatetea vuguvugu la kujitenga bado hawajatambua timu yetu itakosa nguvu kiasi gani," alitania.

Je wajua kwamba mtoto akipewa chakula kigumu mapema analala vizuri?

Watoto wa wahamiaji pia wamewakilishwa vizuri katika upande wa Uingereza.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Timu ya England iliyocheza dhidi ya Sweden imejumuisha watoto wanne wenye wazazi japo mmoja aliye mhamiaji( Nyuma kutoka kushoto) Ashley Young (Jamaica); Dele Alli (Nigeria); (Mbele) Harry Kane (Ireland); Raheem Sterling (Jamaica)

Mafanikio yasiyo tarajiwa ya kikosi cha meneja Gareth Southgate - kikosi chenye wachezaji sita ambao wana angalau mzazi mmoja mhamiaji aliye hamia uingereza na Raheem Sterling ambaye amezaliwa Jamaica - ni mfuasi anayevutia.

"Sisi ni timu ambayo tuna utofauti wetu na vijana tunao wakilisha uingereza ya kisasa. Uingereza tume tumia muda mwingi tukizama katika kutafuta usasa wetu. Najua kwamba kitu cha kwanza nitakacho zungumziwa zaidi ni matokeo ya mpira. Lakini tuna nafasi ya ya kuleta matokeo chanya katika mambo mengine mengi na makubwa," Southgate anaelezea matumaini yake.

Je ni nani huyu aliyevishwa pete ya uchumba na Justin Bieber?

Wanawake Iran wacheza muziki kumuunga mkono binti aliyekamatwa

Lakini wataalamu wa mahusiano ya kimatabaka wanashauri juu ya kuwa na tahadhari.Piara Powar, mwanzilishi wa mtandao wa FARE, shirika linalo shughulikia masuala ya ubaguzi wa rangi katika soka ulaya, anaonya kwamba timu zenye watu wa asili tofauti sikuzote haziwi na matokeo ya kudumu kwa watu.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Raheem Sterling (kushoto) alizaliwa Kingston, Jamaica

"Kua na watu wenye asili tofauti katika timu zote tatu za nusu fainali ni ishara kubwa, lakini uzoefu wa nyuma unaonyesha kwamba matokeo chanya yana dumu kwa miezi michache tu. Hata sasa tunaona mchezaji mwenye rangi ya pekeake katika timu ya uingereza, Raheem Sterling, akichambuliwa katika kila mchezo na wakosoaji," Powar ameiambia BBC.

"Sina uhakika kama Sterling hatokuwa ndio kisingizio cha kufeli kama Uingereza itapoteza katika mchezo wa nusu fainali, kama ilivyotokea kwa mchezaji mwenye asili ya Uturuki Mezut Ozil wakati Ujerumani ilipotolewa nnje katika michuano," Piara anaongeza.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii