Gracious Amani: 'Alicia Keys' wa Kenya apata mkataba na kampuni ya muziki

Gracious Amani aka Amani G Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Gracious Amani aka Amani G

Glorious Amani, Msichana wa eneo la Githurai nchini Kenya aliyelishangaza taifa kwa namna alivyoimba wimbo wa nyota wa muziki kutoka Marekani Alicia Keys amesajiliwa na kampuni ya muziki.

Amani amesajiliwa na kampuni ya Pine Creek Records iliopo jijini Nairobi ambayo imeamua kukuza kipaji chake .

Kampuni hiyo ya muziki ilitangaza habari hiyo njema katika mtandao wake wa facebook.

Akizungumza na BBC kwa njia ya simu, Afisa mkuu wa kampuni hiyo Peter Nduati amesema kuwa msichana huyo atakayetia saini kandarasi ya miaka miwili atazinduliwa rasmi siku ya Ijumaa

Haki miliki ya picha Peter Nduati/ Instagram
Image caption Afisa mkuu wa kampuni ya muziki ya Pine Creek Records Peter Nduati na Amani G

Nduati amesema kuwa mamake msichana huyo atahudhuria hafla hiyo.

''Kipaji chake kimewasili nyumbani ambapo kitakuzwa kwa kiwango cha juu... Jumuika nasi katika kumkaribisha Amani G katika lebo yetu ya muziki'', ulisema ujumbe huo katika mtandao wa Facebook.

Baadaye kanda fupi ya video inamuonyesha msichana huyo akiimba wimbo mmoja wa kiswahili usiojulikana.

Amani aligonga vichwa vya habari mwezi uliopita baada ya video yake inayomuonyesha akiimba wimbo wa nyota wa muziki nchini Marekani Alicia Keys kusambazwa sana mitandaoni.

Alicia Keys baadaye alituma ujumbe wa Twitter kuhusu kanda hiyo ya video akisema ni msichana mrembo.

Mwanamuziki wa Kenya Vivian amerekodi wimbo mmoja naye.

Amani ambaye yuko katika darasa la nane ni mwana wa Wuod Fibi, mwimbaji wa Kenya na mtayarishaji wa muziki. Pia amejipatia jina Amani G.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii