Matukio:Operesheni ya kuwaokoa vijana waliokwama pangoni nchini Thailand

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Mkasa huo uliodumu kwa siku 17 uliligusa taifa zima

Jitihada kubwa za kuwatafuta na kuwaokoa kundi la vijana wa timu ya soka Thailand kutoka pango lililofurika maji liliwagusa watu wengi duniani.

Vijana 12 wa timu ya Wild Boar wenye umri wa kati ya miaka 11-16 waliingia katika mapango ya Tham Luang katika jimbo la Chiang Rai nchini Thailand wakiwa na mwalimu wao mwenye umri wa miaka 25

Baada ya watoto hao kutoonekana nyumbani waliripotiwa kupotea na jitihada za kuwatafuta zikaanza.

Kodi ya mitandao ya kijamii Uganda kuangaliwa upya

Ugonjwa wa zinaa usiosikia dawa

Serikali ya Tanzania yatishia kuiadhibu Twaweza

Waokoaji walipofika katika eneo hilo waliripotiwa kukuta Baikeli, viatu vya kuchezea mpira wa miguu na vitu vingine vilivyokuwa katika eneo la kuingilia pangoni

Haki miliki ya picha AFP/Getty
Image caption Baiskeli karibu na lango la pango
Haki miliki ya picha EPA
Image caption Watu wamekusanyika kwa ajili ya kupata taarifa,pembeni ni taa kwa ajili ya kuangaza pangoni

Vyombo vya habari na watu waliojitolea wameanza kukusanyika wakati ambapo mvua kubwa ikiendelea kunyesha na kuletea changamoto juhudi za utafutaji na uokoaji.

Siku ya Jumapili familia zalifika eneo la pangoni wakisali na kukesha kwa ajili ya watoto waliopotea.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Mwanamama akisali huku akiwa amejifunika plastiki nje ya pango

Siku ya tatu, wapigambizi wa kikosi cha jeshi la wanamaji waliwasili kusaidia shughuli ya uokoaji

Waokoaji walitafuta njia mbadala za kuingia kwenye pango na mamlaka ilifikiria kupasua miamba ili kupata njia ya kuingia ndani.

Haki miliki ya picha AFP/Getty
Image caption Baiskeli karibu na lango la pango
Haki miliki ya picha AFP/Getty
Image caption Wanajeshi wakitandika nyaya za umeme pangoni

Wataalamu wa kupiga mbizi kutoka duniani kote waliwasili nchini humo kwa ajili ya kusaidia waokoaji.

Familia ziliendelea kukesha wakiomba katika eneo hilo.Wanafamilia na maafisa walionekana wakizirai na hofu ikiongezeka huku hali ya hewa ikiwa mbaya

Haki miliki ya picha Twitter/@namwoon_ccw
Image caption Picha ya vikaragosi vikionesha watoto wakiwa wamewakumbatia waokoaji

Pampu ziliwekwa kwa ajili ya kupunguza kina cha maji kwenye pango, lakini haikufua dafu kutokana na mvua kubwa iliyokuwa ikinyesha.

Mtanzania aliyechangia kuunda ndege ya Dreamliner

Marekani imeshindwa kuwarejesha watoto wa wahamiaji kwa wazazi wao

Waokoaji sasa wanaamini na matumaini kuwa wavulana watakuwa salama ndani ya pango.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Mzazi akionekana mwenye huzuni
Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Waziri Mkuu akiwasikiliza walezi

Waziri Mkuu Prayuth Chan-ocha anawatembelea walezi katika eneo hilo na kuwafariji, akiwaambia,:''Ni vijana shupavu.wana nguvu''.

Vyombo vya habari vya ulimwenguni vimekusanyika kwa ajili ya kufahamu kinachojiri.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Mfanyakazi wa kikosi cha anga akiteremka kutoka kwenye helikopta

Hali ya hewa imetulia, inawaruhusu waokoaji kuingia zaidi ndani ya pango.

vifaa na mitungi ya hewa yanaingizwa ndani ya pango.

Haki miliki ya picha AFP/Getty
Image caption Wataalamu wakibeba pampu za maji katika eneo la pango

Siku ya Jumatatu kuna habari njema-waokoaji wamewapata vijana wote na mwalimu wao wakiwa salama, siku tisa baada ya kupotea.

Haki miliki ya picha Royal Thai Navy
Image caption Video ilitolewa kuonyesha waokoaji wa Uingereza walipowaona wavulana
Haki miliki ya picha AFP/Getty
Image caption Ni shangwe kwa wazazi na maafisa walipopokea habari njema

Picha za Video ziliwaonyesha vijana wakiwa na afya njema, lakini maafisa wanasema zoezi lilikuwa gumu sana.

Mamilioni ya lita za maji yalitolewa kutoka kwenye mapango, lakini kutokana na mvua, maafisa waliwaasa vijana wanapaswa kujifunza kuogelea au wasubiri kwa miezi kadhaa mpaka hali ya hewa itakapotengamaa.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Trekta na vifaa vingine vikionekana katika eneo la pango
Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Matangi ya hewa ya oksijeni yakiwa nje ya pango

Hali ya simanzi ilijitokeza mwishoni mwa juma baada ya muokoaji mmoja aliyekuwa kwenye operesheni ya uokoaji alipofariki.

Saman Gunan, mfanyakazi wa zamani wa kikosi cha majini alikuwa akijitolea pangoni, alipoteza fahamu walipokuwa anapeleka mitungi ya oksijeni

Haki miliki ya picha Reuters

Salamu za rambirambi kutokana na kifo chake zilitolewa, huku kukielezwa kuwa zoezi la uokoaji litakuwa gumu

Hatimaye iliripotiwa vijana wanne walifanikiwa kutolewa nje.

Maafisa wanasema operesheni inakwenda vizuri, lakini jitihada zitasimama kwa muda ili waokoaji wapate muda wa kupumzika na kubadili mitungi ya oksijeni

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Magari ya kubaba wagonjwa yakiondoka huku yakitazamwa na vyombo vya habari

Operesheni ni ngumu sana, inahusisha kutembea, kutambaa, kupanda na kupiga mbizi.

Wavulana 4 zaidi waliokwama pangoni Thailand 'waokolewa'

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Wanafunzi wenzao wakifurahia taarifa kuhusu shughuli za uokoaji zinavyoendelea

Wavulana wako hospitali kwa ajili ya uangalizi.Nafasi ya wazazi kuwatembelea imezuiwa kwa muda kwa sababu za tahadhari za kitabibu.

Siku ya Jumanne kuna matumaini kuwa shughuli ya uokoaji itafanikiwa, kukitarajiwa kupatikana wengine ambao bado wapo ndani.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Wananchi wakipungia gari ya kubeba wagonjwa ilipokuwa ikitoka kwenye eneo la pango

Jitihada zinaendelea siku nzima ya jumanne mpaka pale Wavulana wote na kocha wao waliokwama pangoni Thailand waokolewa

Wananchi na waokoaji wanashangilia, wakati vijana na mwalimu wao wanapopelekwa hospitalini, siku 17 baada ya kunasa pangoni.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Watu wakishangilia huku wengine wakitazama kwenye runinga
Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Msichana akiwa amevalia kofia yenye alama ya timu ya Wild Boar, ambayo sasa imekuwa maarufu

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii