Mamake Diamond Sandra amtambua Daylan, mwana wa Hamisa Mobetto kuwa mjukuu wake

Diamond Platinumz Haki miliki ya picha Getty Images/AFP

Mamake mwanamuziki nyota Afrika mashariki Diamond Platnumz Bi Sandra hatimaye amemtambua mjukuu wake wa tatu aliyezaliwa na mwanamitindo Hamisa Mobetto kutoka Tanzania

Bi Sandra amedaiwa kukataa kutambua uhusiano wa mwanawe na Hamisa Mobetto, hatua iliomfanya Diamond kumuomba mamake hadharani kuwapenda wajukuu wake wote kwa usawa.

Na wakati wa siku yake ya kuzaliwa , bi Sandra alirekodiwa katika kanda ya video akisema, ''Si Dylan ni mume wangu''?.

Familia yake ambayo ilikuwa imekusanyika katika hafla hiyo ya kukata keki walimpigia makofi wakisherehekea.

Bi Sandra baadaye aliendelea na kukata keki ya Dylan ambayo alikuwa ameletewa kusherehekea siku hiyo ya kuzaliwa kwake.

Sandra hupendelea sana kuchapisha kanda za video na picha za wajukuu wake wawili Tiffa na Nillan waliozaliwa na mfanyibiashara wa Uganda Zari Hassan.

Amekuwa akikosolewa kwa kumpuuza Daylan na kutochapisha picha zake katika akunti yake.

Huwezi kusikiliza tena
Diamond Platinumz azungumza na Salim Kikeke: Mahojiano kamili

DIAMOND Alivyoingilia kati

Ilimlazimu mwanawe Diamond kuingilia kati kwa yeye kuweza kumtambua mwana aliyezaliwa na Mobetto.

Katika chapisho lake la mtandao wa instagram Diamond alimrai mamake kuwapenda wajukuu zake wote bila upendeleo wowote akisema kuwa hawana hatia wala hawajui chochote.

Haki miliki ya picha Diamond/Instagram
Image caption Diamond na mwanawe Daylan

Aidha alimtaka bi Sandra kutojiingiza katika maswala ya kibinafsi kati yake na mama za wajukuu zake akisema kuwa yeye ndio wa kulaumiwa kwa hayo yote.

Vilevile aliwataka mashabiki wake kutopendelea upande wowote katika swala la wanawe watatu akisema wote ni wake na kwamba hakuna anayepaswa kumtenga mwana wa Mobetto.

Hivi ndivyo alivyoandika katika mtandao wake wa Instagram:

"Diamond Platnumz: I can't Stop Wishing you Happy Birthday Mom... Coz i Love you So Much, na Najua kias gani pia Unanipenda Mwanao, Unanipenda kias kwamba hata Unachukia yoyote anaejaribu kufanya kitu cha kuniharibia Katika Maisha Yangu...Utanilinda na kunitetea Hata kama pengine mgomvi nilikuwa ni mimi Mwanao, ila you will always be on my side......Katika Kusheherekea siku yako hii kuu ya kuzaliwa, ningeomba Pia, kama Unipendavyo Mwanao pia Uwapende wajukuu zako wote, kwani ni wadogo na Hawana hatia wala hawajui chochote...Najua wakati mwingine wazazi wao wanakukwazaga sana, kutokana na Issue zetu Binafsi za mimi na wao kukuingiza wewe ama kukuletea lawama wewe ilhali maskini ya Mungu hata napowatoaga hujui, unaonaga tu na wewe ghafla niko na flani.... na kwa umri nilofikia hata kama hupendezwi kias gani, ila huwezi nichapa viboko ama kunicontrol kuwa eti kwanini niko na fulani....hivyo ni kosa langu mimi binafsi ila wao wanatakaga kukupa lawama kama wewe jaji wa mahusiano yangu... ila kwa Upendo wako kwangu naomba Unisamehe mie kwani ndie Chanzo cha Hayo yote... na Uwapende Wajukuu zako wote kwani ni watoto na hawajui chochote.....Na wakukwazapo Wazazi wao Wakuwahukumu wao hata wakitumia ngao ya watoto kukukwaza.......Watu wa Mitandaoni watasheherekea na kuunda timu kwa faida za Mam za watotoila si kwa faida za watoto maana hakuna hata mkoja alowai nichangia hata ela ya pempaz kwanhawa watoto, na wakimaliza kuchonganisha familia yetu kupitia mitandao, wao wanarudi makwao kukaa na nafamilia zao huku weww wnakutengenezea matabaka katika familia yao.....Mama angu kipenzi familia nilokuletea Mwanao ni @deedaylan @princess_tiffah @princenillan , hao ndio familia yako tokea kwangu, na siku nikioa huyo ndio atakuwa mwengine kwenye Familia..... Nakupenda sana na Nakutakia Maisha maref yenye furaha na Afya Tele MamaπŸ’•πŸ’–πŸ’•πŸ’–@mama_dangoteπŸ’•πŸ’–πŸ’•πŸ’–"

Haki miliki ya picha Diamond/Instagram

Tayari baadhi ya mashabiki wake wamepongeza hatua hiyo ya mamake kumkubali mjukuu wake wa tatu licha ya uhusiano wake na Mobetto.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii