Kylie Jenner: Dadake Kim Kardashian kuwa bilionea mwenye umri mdogo zaidi duniani

Kylie Jenner Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Midomo ya Kylie Jenner ilimsaidia kuanzisha chapa yake ya vipodozi

Nyota wa zamani wa kipindi cha Keeping Up with the Kardashians Kylie Jenner ana thamani ya $900m akiwa na umri wa miaka 20 , kulingana na Forbes.

Jarida hilo la biashara limesema kuwa nyota huyo wa mtandao wa kijamii anaelekea kuwa bilionea mwenye umri mdogo duniani.

Nyota huyo wa mitindo ambaye , ndio mwana mdogo wa familia ya Kardashian , alizindua kampuni ya vipodozi miaka miwili iliopita.

Akilinganishwa na dada yake wa kambo , Kim Kardashain West mwenye umri wa miaka 37, thamani ya msichana huyo imeipiku ile ya dadake mkubwa kwa takriban $350m.

Jenner ambaye hajafikisha miaka hata ya kunywa pombe nchini Marekani atafikisha umri wa miaka 21 mnamo mwezi Agosti , huku toleo jipya la jarida la Forbes lenye picha yake katika ukurasa wa mbele likitolewa.

Kile ambacho dadake Kim Kardashian West alifanyia upasuaji ili kuongeza makalio yake, Jenner alifanyia upasuaji midomo yake ili kuongeza ukubwa wake, Forbes iliandika , ikielezea umaarufu wake.

Mapema wiki hii Jenner-mama ya mtoto mmoja wa kike kwa jina Stormi alitangaza kuwa atasita kudungwa sindano za kuongeza ukubwa wa midomo yake , kwa jina Dermal Fillers.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Kylie Jenner amesitisha sindano za kumuongeza midomo yake

Jenner alikiri katika kipindi kimoja cha Keeping Up With The Kardashians mwaka 2015 kwamba midomo yake imekuwa kitu ambacho kimekuwa kikimshusha hadhi hivyobasi angependelea kubadilisha ili kuongeza ukubwa wake.

Baadaye alizindua chapa yake ya vipodozi kwa Jina Kylie Cosmetics , ambayo ilishirikisha msururu wa bidhaa za midimo.

Upasuaji wake wa midomo ulivumbua mtindo mpya ambao umewafanya wasichana zaidi kuomba midomo yao kuongezwa ukubwa kulingana na madaktari wa upasuaji.

Kampuni ya Jenner anayomiliki ina thamani ya $800m, kulingana na Forbes.

Ameorodheshwa na Forbes katika nafasi ya 27 ya wanawake waliojitengezea utajiri nchini Marekani, akimpiku Barbra Streisand ($400m), Beyonce Knowles ($335m) na Taylor Swift ($320m).

Jenner anaelekea kuwa bilionea mapema zaidi ikilinganishwa na Mark Zuckerberg, mwazilishi wa mtandao wa facebook, ambaye alifanikiwa kuwa bilionea akiwa na umri wa miaka 23.

Evan Spiegel, mmiliki wa Snapchat, pia alikuwa bilionea katika miaka yake ya 20 , lakini bado haijulikani ni vipi aliafikia hilo

"wow. siamini jarida la Forbes litakuwa na picha yangu," aliandika katika mtandao wake ulio na wafuasi milioni 110 siku ya Jumatano.

"Ahsante kwa makala hii na kutambulika. Nimebarikiwa kufanya kile ninachopenda kila siku. Sikudhania kwamba hili linaweza kufanyika''.

Tovuti ya Dictionary.com ilituma ujumbe katika twitter kuhusu habari hiyo ya Forbes:: "kujifanikisha kunaamanisha kufanikiwa katika maisha bila usaidizi."

Jenner mara ya kwanza alijipatia umaarufu akiwa na umri wa miaka 10 wakati alipoonekana na familia yake katika kipindi hicho chaKeeping up with the kardashian

Katika mitandao ya kijamii, watumiaji kadhaa waliikosoa Forbes kwa kutumia neno ''alijijenga", akidai kwamba wazazi wa Jenner tayari walikuwa matajiri na maarufu.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii