Katarina Zarutskie: Mwanamitindo aliyeng'atwa na papa akipiga picha naye kisiwa cha Exuma nchini Bahamas

Katarina akisimama katika bembea juu ya maji
Maelezo ya picha,

Katarina amtusiwa mtandaoni kufuatia picha za shambulio hilo

Kisiwa cha Exuma nchini Bahamas kina umaarufu wa michanga meupe iliopo ufuoni mwa bahari , maji masafi na maneo mengi ya kuvutia.

Hivyobasi mwanamitindo Katarina Zarutskie alipozuru ufuo huo pamoja na mpenzi wake, mwezi uliopita alikuwa na ari ya kutumia maeneo mazuri ya fukwe hiyo ya bahari.

Baada ya chakula cha mchana na familia katika eneo linalojulikana kama Staniel Cay, Katarina aliwaona watu waliokuwa wakiogelea karibu na papa mchanga katika eneo moja.

Licha ya familia ya mpenzi wake kuwa na wasiwasi, alikuwa yuko tayari kuingia katika maji hayo ili kupiga picha nao.

'Mwana wa bahari'

Msichana huyo mwenye umri wa miaka 19 anatarajiwa kuanza mafunzi ya shahada mbili za uuguzi na biashara mjini Miami na sio mgeni wa maswala ya bahari baada ya kukuwa akifanya michezo ya baharini nyumbani kwao huko mjini California.

''Kutokana na ufahamu wangu wa kuteleza majini na kuogelea chini ya maji najua kwamba papa wachanga huwa salama'', aliambia BBC .

Nimeona watu wengi wakipiga picha nao katika mtandao wa Instagram

Samaki huyo amekuwa kivutio cha watalii, akizurura katika gati mbali mbali na kuonekana katika maelfu ya picha zilizosambazwa katika mitandao.

Anasema kwamba baada ya dakika chache za kuchukua mkao , raia mmoja wa eneo hilo alimshawishi kuolea majini huku mwili wake ukiangalia juu.

''Wakati huo watu walikuwa wameanza kupiga picha , nilipokuwa nikilala kuangalia juu nilihisi kitu kimenivuta chini'', alisema.

Babake mpenzi wake alikuwa akimpiga picha Katarina wakati huo, na kwa bahati nzuri akapata kisa chote katika kamera yake.

Maelezo ya picha,

Wakati papa huyo alipomuuma picha hiyo ilipigwa na familia ya mpenzi wake

Maelezo ya picha,

Katarina alipigwa picha akitaabika katika maji, akijaribu kujiokoa

Maelezo ya picha,

Picha za mitandao ya kijamii zinaonyesha kuwa watu wengi wamepiga picha na papa huyo katima eneo hilo la watalii

[Onyo: Baadhi ya picha zinaogofya]

Papa huyo alimzuilia chini ya maji kwa sekunde chache kabla ya kuamua kuondoa kiganja chake cha mkono katika mdomo wake.

Picha hizo zinamuonyesha akifunika jereha hilo na kuinua mkono wake katika juhudi za kuzuia damu kuenea katika maji .

"Wakati huo mwili wako una wasiwasi mwingi na hatua ya pekee ni kujiondoa katika hali hiyo, lakini nilitulia'' ,anasema.

"Nadhani iwapo mtu angepiga kelele na kuinua mikono akitafuta usaidizi hali ingebadilika "

Katarina alilazimika kushonwa na kupewa dawa , na bado ana vipande vya meno vya papa huyo vilivyosalia katika kidonda hicho.

Jeraha hilo la meno litawacha kovu baya , lakini mwanamitindo huyo alisema kwamba anahisi amebarikiwa kwamba tukio hilo halikuwa baya sana.

Maelezo ya picha,

Katarina anasubiri kuona iwapo atahitaji upasuaji kuondoa vipande vya meno

Tangu habari yake kuchapishwa katika vyombo vya habari vya Marekani , Katarina amepokea maelfu ya mashabiki katika mtandao ikiwemo shutuma chungu nzima

'Mwanamitindo mjinga wa instagram'

Amekasirishwa na vile alivyodaiwa anapenda sana mitandao ya kijamii bila tahadhari yoyote.

Mwanamitindo huyo hakupanga kupakia picha hizo katika akaunti zake za mitandao ya kijamii hadi alipofuatwa na waandishi kuhusu uzoefu wake wiki hii.

Katarina pia amepinga madai kwamba alipuuzilia mbali ushauri wa wenyeji na kuingia majini wakati wa saa za kulishwa kwa wanyama hao.

''Walichukua habari walizotaka na kuchapisha kwa njia ambayo zilinifanya kuwa mwanamitindo mjinga katika instagram'', alisema.

Nimepokea maoni ya ujeuri na ya chuki kutoka kwa wayu ambao walikuwa wakisema vitu vya kushangaza.

Maelezo ya picha,

Mpenzi wake Katarina Nicolò amekuwa akisaidia kufuta matusi katika kurasa zake za mitandao ya kijamii