Stormy Daniels: Nyota wa filamu za ngono aliyemtishia Trump akamatwa Ohio

Stormy Daniels, real name Stephanie Clifford, standing outside a shop in West Hollywood May 2018 Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Bi Daniels alijikuta kwenye mfarakano na Rais Donald Trrump baada ya kusema kuwa alifanya mapenzi naye mwaka 2006 madai ambayo Trump anayakataa.

Nyota wa filamu za ngono nchini Marekani Stormy Daniels amekamatwa kwenye klabu moja ya burudani huko Ohio, kwa mujibu wa wakili wake.

Bi Daniels alikamatwa kwa madai kuwa alimruhusu mteja kumgusa jukwaani, "kwa njia ambayo haikuwa ya kingono," wakili Michael Avenati aliandika katika twitter.

Bi Daniels alijikuta kwenye mfarakano na Rais Donald Trrump baada ya kusema kuwa alifanya mapenzi naye mwaka 2006 madai ambayo Trump anayakataa.

Wakili wake alitaja kukamatwa huko kama mtego ulikochochewa kisiasa.

Bw Avenatt aliandika katika twitter kuwa Bi Daniels ambaye jina lake kamili ni Stephanie Clifford, alikuwa akicheza mtindo ambao amekuwa akiucheza kote nchini kwenye karibu vilabu 100.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Stormy Daniels alijikuta kwenye mfarakano na Rais Donald Trrump baada ya kusema kuwa alifanya mapenzi naye mwaka 2006 madai ambayo Trump anayakataa.

Alisema alitarajia aachiliwe kwa dhamana na afunguliwe mashtaka akisema kuwa atayapinga mashtaka yote.

Sheria ya Ohio inayojulikana kama Community Defense Act inamzua mtu yeyote kumgusa mcheza densi kwenye klabu kama hawahusiani.

Klabu ya Sirens iliandika katika twitter mwezi uliopita ikisema kuwa Daniels angefika katika klabu hiyo usiku wa tarehe 11 na 12 mwezi huu.

Bi Daniels anasema alilipwa dola 130,000 muda mfupi kabla ya uchaguzi wa urais wa mwaka 2006 kukaa kimya kuhusu madai ya uhusiano wake wa kimapenzi na Bw Trump.