Mwanamume achapwa viboko 80 kwa makosa aliyoyatenda akiwa miaka 14 Iran

File photo showing an Iranian police car in Tehran (10 April 2018) Haki miliki ya picha AFP
Image caption Uzinzi, kupiga busu hadharani, wizi, vitendo vinavyohusiana na mapenzi ya jinsia moja na kufuru yote hayo yanaweza kusababisha mtu kuchapwa viboko nchini Iran

Amnesty International imelaani mamlaka nchini Iran kwa kumchapa viboko hadharania mwanamume ambaye alipatikana na hatia ya kunywa pombe wakati alikuwa na umri wa miaka 14.

Vyombo vya habari vilichapisha picha za mwanamume ambaye alitambuliwa kama "M R" akichapwa viboko 80 kwenye mji ulio mashariki wa Kashmir siku ya Jumanne.

Waendesha mashtaka wanasema alikamatwa wakati wa maadhimisho ya mwaka wa Iran wa 1385 wa kati ya (Machi 2006 na Machi 2007) na alihukumiwa mwaka uliopita.

Haijulikani sababu iliyochangia adhabu hiyo kuchukua zaidi ya miaka 10 kutekelezwa.

Picha hizo zinaonyesha mwanamume akiwa amefungwa kwenye mti akichapwa na mtu ambaye amejifunika uso. Umati mdogo wa watu nao wanaonekana wakitazama kwa mbali.

Mwaka 2014 raia sita wa Iran walihukumiwa jela na viboko 91 baada ya kukamatwa baada ya kuonekana wakiuchezea densi wimbo wa Pharrel Williams.

Mambo yanayoweza kusababisha uchapwe viboko Iran

Uzinzi, kupiga busu hadharani, wizi, vitendo vinavyohusiana na mapenzi ya jinsia moja na kufuru yote hayo yanaweza kusababisha mtu kuchapwa viboko nchini Iran. Wale wanaoptikana na hatia uhukumiwa kati ya viboko 10 na 100 mgongoni kwa kutumia fimbo ya urefu wa futi tatu.

"Uchungu ni mwingi na hata watu huzirai baada ya kuchapwa vikobo saba au nane," anasema Anicee Van Engelan mtaalamu wa sheria ya Iran kwenye chuo cha masuala ya Afrika cha London.

Mwandishi wa BBC idhaa ya kiajemi anasema kuwa adhabu kama hiyo ilikuwa inafanyiwa maeneo ya umma ili kumtia aibu yote yule ambaye anaadhiniwa lakini kwa sasa inaweza kufanyiwa kwenye vituo vya polisi.

Mada zinazohusiana