Wabunge Kenya wamekwenda kuangalia kombe la dunia kwa gharama ya nani?

Millicent Omanga Haki miliki ya picha Millicent Omanga
Image caption Seneta Millicent Omanga alitazama mechi ya nusu fainali kati ya Croatia-England

Wakenya wamekasirishwa na taarifa kwamba wabunge 20 wamesafiri kwenda Urusi kutazama kombe la dunia kwa gharama ya fedha za umma.

Wamekwenda kutazama mechi nne, ikiwemo fainali kati ya Ufaransa na Croatia, katika safari ya wiki mbili inayokadiriwa kuwa na thamani ya maelfu ya dola.

Mjadala ulizuka baada ya wabunge hao kuweka picha walizopiga uwanjani.

Waziri wa michezo Rashid Echesa ameiambia BBC kwamba alitoa idhini kwa wabunge 6 pekee kusaifiri, kusaidia kuelewa jinsi matukio makubwa ya kimataifa yanavyoandaliwa.

Kenya haijawahi kufuzu kwa fainali ya Kombe la Dunia na imeorodheswha nafasi ya 122 kati ya matifa 206 na shirikisho la soka duniani FIFA.

Hatahivyo Kenya ina umaarufu mkubwa katika riadha na ni mojawapo wa mataifa yenye ufanisi mkubwa duniani .

Tayari nchi hiyo imewasilisha ombi la kutaka kuwa mwenyeji mashindano ya kimataifa ya riadha mwaka 2023.

Lakini hisia iliopo kwa Wakenya ni kwamba safari hiyo ni upotezaji wa fedha za umma katika nchi ambayo kipato cha mtu wa kawaida ni $150 kwa mwezi.

Katika maoni yaliopo huyu anastaajabishwa na hatua hiyo akieleza kwamba huwezi kuwaona viongozi wakitazama hata mechi za ndan ya nchi kuinusha talanata ya ndani lakini wabunge wana muda wa kujigamba kwa picha Urusi.

Huyu naye anahoji sababu iliotolewa, kwamba 'ni jukumu lao kuelewa michezo na namna ya kuandaa matukio makubwa ya kimataifa', anauliza je wabunge hao watakuwepo madarakani wakati na iwapo Kenya itaanda michezo kama hiyo?

Miwngine akachukua fursa kuzungumzia deni linaloongezeka la nchi lakini licha ya hayo bado wabunge wanakwenda kutazama Kombe la Dunia.

Seneta Millicent Omanga, ni mmoja ya waliosafiri kwenda Urusi na katika picha aliobandika anaonekana kufurahia kuwepo katika michuano hiyo.

Lakini kiongozi wa tume ya huduma za bunge Kenya Jeremiah Nyegenye, ambayo tume hiyo ndio hubaini majukumu na malipo ya wabunge ameeleza kwamba safari hiyo ina manufaa.

"Ni jukumu lao kuelewa michezo, namna ya kuandaa mashindano ya aian ahiyo ya kimataifa," gazeti la The Star newspaper limemnukuu. " Huu sio wakati wa kustarehe na sio sawa kuitazama tu kama safari ya kwenda kupteza wakati."

Malipo na marupurupu ya wabunge Kenya

Duru kutoka ndani ya bunge ameiambia BBC kwambakwa kawaida wabunge husafiri kiwango cha watu wa mashurhui au first class.

Wanapokuwa katika safari za kazi, wabunge Kenya wanastahili kulipwa marupurupu ya matumizi ya kila siku kiasi ya $1,000.

Inaaminika kwamba wabunge wa kenya ni miongoni mwa wanaolipwa vizuri zaidi duniani lakini mwaka jana walikatwa mishahara kwa 15% na kuishia na mshahara wa $6,100 kwa mwezi.

Mishahara mipya

 • Rais: Sh1.4 milioni kutoka Sh1.65 milioni
 • Naibu Rais: 1.2 milioni kutoka 1. 4 milioni
 • Mawaziri: Sh924,000 kutoka Sh1.056 milioni
 • Makatibu wa Wizara: Sh765,000 kutoka Sh874,000
 • Magavana: Sh924,000 kutoka Sh1.056 milioni
 • Wabunge: Sh621,000 kutoka Sh710,000
 • Maspika: Sh1.155 milioni kutoka Sh1.30 milioni
 • Naibu Spika: Sh924,000 kutoka Sh1.006 milioni
 • Viongozi wa Serikali na Upinzani Bungeni: Sh765,000 kutoka 1.020 milioni
 • Madiwani (Wawakilishi wa Wadi): Sh144,000 kutoka Sh165,000
 • Mawaziri wa Serikali za Kaunti: Sh259, 875 kutoka Sh350,000
 • Mishahara ya viongozi wa mataifa makuu duniani

Katika makato hayo yalioidhinishwa wabunge Kenya walipoteza marupurupu waliokuwa wakipata kama vbile ya usafiri na kuhudhuria vikao vya bunge.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii