''Mwanamume afunguka kuhusu hatua yake ya kufunga njia ya uzazi''

'Michael' ameiambia BBC alichagua kufunga uzazi baada ya mkewe kupata maumivu makali kutokana na sindano za uzazi wa mpango
Image caption 'Michael' ameiambia BBC alichagua kufunga uzazi baada ya mkewe kupata maumivu makali kutokana na sindano za uzazi wa mpango

Michael ni mmoja kati ya wanaume wachache wa kiafrika kufunga uzazi, lakini anasikitika .

Anaiambia BBC namna ambavyo tamaduni za kiafrika zinavyodanya iwe vigumu kuzungumzia kuhusu taratibu hizo ambazo wataalamu wanaamini zinaweza kuwa suluhu ya changamoto ya ongezeko la watu kupita kiasi barani afrika

''Nilitaka iwe zawadi kwa mke wangu, kujitoa'', anaeleza.

''kumuonyesha kuwa ninampenda kweli na kuwa naweza kwenda mbali zaidi kufanya jambo kubwa lisilofikirika''

Michael(Jina la kubuni) alifunga uzazu miezi michache iliyopita, lakini hakuwahi kumwambia mtu yeyote isipokuwa mkewe

Nitachukia sana ikiwa mtu mwingine atajua. Kuna hali ya unyanyapaa na sitaki watu wanihukumu au kuingilia maisha yangu mwenyewe'', kijana huyo mwenye miaka 34 anaeleza kwa nini hataki kujulikana kwenye makala haya.

Tofauti na Ulaya na Marekani, kufunga uzazi kwa wanaume wa Afrika kunaleta hali ya hofu kwao.


Ufungaji wa kizazi kwa wanaume ni nini?

Haki miliki ya picha tzahiV/Getty Images
Image caption Maana ya Vasectomy kwenye kamusi

Njia ya kufunga uzazi kwa wanaume ni njia ya uzazi wa mpango ambayo hufanywa kwa njia ya upasuaji kukata au kufunga mirija inayosafirisha mbegu za uzazi za mwanaume, ili kuzuia mwanamke asipate mimba.

Upasuaji mara nyingi hufanywa kwa muda wa dakika takriban 15, mgonjwa huwa macho lakini huwa hapati maumivu yeyote.

Njia hii inafanya kazi ya kuzuia mimba kwa silimia 95.

Njia ya kufunga uzazi kwa wanaume haiathiri nguvu za kiume au uwezo katika tendo au kulifurahia tendo.Mwanaume ataweza hayo yote,isipokuwa hataweza kumpa mwanamke ujauzito.

Njia hii haizuii mwanaume dhidi ya maradhi ya zinaa, kama mipira ya kiume ambayo inaelezwa kuwa njia ya kuaminika kwa asilimia 98 ikiwa itatumika vyema.


Asilimia ndogo sana ya wanaume wa kiafrika wamefunga uzazi, hii ni kwa mujibu wa ripoti ya Umoja wa mataifa ya mwaka 2013.

Nchini Afrika Kusini na Namibia idadi ni kubwa kwa 0.7% na 0.4%. Duniani kote, 2.2% ya wanaume wamefunga uzazi ukilinganisha na 18.9 % ya wanawake waliofunga uzazi.

Lakini Michael anasema hakuacha utamaduni kuingilia maamuzi yake ya kumpunguzia maumivu mke wake kutokana na sindano za uzazi wa mpango.

Tayari wana watoto watatu, anasema ahitaji watoto zaidi.

''Alikuwa akipata madhara kutokana na sindano, kama vile maumivu anapobeba vitu,'' anaongeza.''Ngozi yake ilikuwa kavu na isiyo laini, na alikuwa akipungua uzani haraka sana''.

Huwezi kusikiliza tena
Jinsi upasuaji unavyofanyika

Mke wake anasema anaweza kuishi bila kuwa na wasiwasi wa kupata watoto ambao hakupangilia

Lakini ana hofu kuwa jamii yake siku moja itagundua, hii ndio sababu ameamua kufanya siri. Alishangazwa na maamuzi ya mumewe.

''Sikuamini kama angefanya hivi kwa ajili yangu kwa sababu hakuna mwanaume wa kiafrika anayeweza kufanya jambo hilo''.Aliiambia BBC.

''Mahali tunapotoka watu husema wanaume wanapaswa kuwa na watoto wengi iwezekanavyo''.

''Wanaume mashujaa''

Moja ya sababu waafrika hawaungi mkono njia hii, kwa mujibu wa wataalamu, ni kuwa wanaume wengi hawana ufahamu kuhusu hili.

''Watu wengine wanafanisha na kuhasiwa, kwa kuwa wanafikiri viungo vyote vinakatwa na kubaki kama mwanamke,'' anaeleza Dokta Charles Ochieng mtaalamu wa masuala ya ufungaji uzazi kwa njia ya upasuaji.

Haki miliki ya picha AFP/SONNY TUMBELAKA
Image caption Madaktari wakifanya upasuaji nchini Indonesia

Kampeni ya kufunga uzazi mwaka huu nchini Kenya kulishuhudiwa wanaume wengi wakijitokeza.

Njia za uzazi wa mpango ni suala ambalo limeachiwa wanawake.Lakini wakati wa siku nne za utoaji elimu , Taasisi isiyo ya kiserikali iliwaita wanaume 100 ''majasiri''

takriban wanaume 70 walijitokeza, wengi wao hawakutaka kutambulika.Michael anasema wazazi wake hawakuweza kuwahudumia milo mitatu kwa siku kwa ajili yake na nduguze watatu

Chakula cha usiku kilikuwa cha kugombewa na familia nzima

''Nitatoka kwenye famili kubwa sana naniliona jinsi wazazi walivyokuwa wakihangaika katika kutulea,'' aliongeza ''Sikutaka kupita njia hiyo hiyo''.

Baba huyu wa watoto watatu anasema upasuaji ulichukua dakika 20 na maumivu yalikuwa kidogo sana, kiasi kwamba aliweza kurejea kazini siku hiyohiyo

''Si mwanaume kamili''

Michael anasema wanaume wanapaswa kuelimishwa kabla ya kuchukua hatua

''Baadhi ya watu wanafikiri kuwa hautakuwa mwanaume kamili baada ya kufanyiwa upasuaji'', aliiambia BBC.

Dokta Ochieng anasema kuna madhara kidogo.

Mwanaume atapata maumivu kidogo baada ya upasuaji na hapaswi kubeba vitu vizito kwa takriban siku mbili.

Ni aghalabu kwa upasuaji huu kutofanikiwa, mwanamke mmoja kati ya 500 hupata mimba isiyotarajiwa baada ya mwaka unaofuata baada ya uapasuaji wa mwenza wake.

Image caption Chati inayoonyesha idadi ya watu wanaofahamu njia hii ya uzazi wa mpango

Hii ni tofauti na mataifa tajiri kama Canada, ambapo mwaka 2013 Umoja wa mataifa ulibaini kuwa 22% ya wanawake walio katika umri wa kuzaa ambao wameolewa wako na wanaume waliofunga uzazi kama njia ya uzazi wa mpango.Nchini Uingereza ni 21% New Zealand ilikuwa 19.5% na Marekani ilikuwa 11%

Nchini Kenya, 38% ya wanawake na 48% wanaume wamesikia kuhusu njia hii ya uzazi wa mpango kwa mujibu wa utafiti wa mwaka 2014.

Katika utafiti nchini Nigeria ilibainika kuwa 16% ya wanawake walioolewa na 27% ya wanaume waliooa wanafahamu kuhusu njia hiyo.Liberia 20% kwa wanawake na wanaume.

Rwanda imewahamasisha wanaume waanze kufikira njia hii tangu mwaka 2011 ili kudhibiti ongezeko la watu katika nchi hiyo ndogo.

''Watu watakaotaka kujiunga na programu hiyo ya uzazi wa mpango wataruhusiwa kufanya upasuaji'', Alisema waziri wa afya wa wakati huo.

Pamoja na kuwa kumekuwa na uhamasishaji, Michael hatarajii kuona idadi kubwa ya wanaume wa kiafrika wakipanga mstari kwa ajili ya upasuaji huo siku za karibuni.

Mada zinazohusiana