Tetesi za soka Ulaya: Antonio Conte, Gareth Bale, Eden Hazard, Willian, Adrien Rabiot na Yerry Mina

Antonio Conte

Chelsea itamlipa mkufunzi wake Antonio Conte fidia ya £9m baada ya kumfuta kazi raia huyo wa Itali ili kumpa fursa aliyekuwa kocha wa Napoli Maurizo Sarri kusimamia timu hiyo. (Mail)

Real Madrid inaandaa dau la £150m kumnunua Eden Hazard, 27, kutoka Chelsea msimu huu. (Mail)

Chanzo cha picha, Getty Images

The Blues wanashindana na PSG kumsaini beki wa AC Milan Leonardo Bonucci, 31. (Corriere dello Sport - in Italian)

Chelsea imepokea ombi la pili kutoka Barcelona kumnunua winga wa Brazil Willian, 29, aliye na thamani ya £60m. (Mail)

Tottenham iko tayari kumuuza beki wake Toby Alderweireld ,29, kabla ya msimu mpya wa ligi ya Uingereza na itatafakari kuhusu makubaliano na Manchester United. (Yahoo Sport)

Mkufunzi wa Liverpool Jurgen Klopp amepinga uwezekano wowote wa kumsaini kipa mpya msimu huu. (Mirror)

Chanzo cha picha, Rex Features

Mshambuliaji wa Real Madrid anayelengwa na Manchester United Gareth Bale, 28, atafanya mazungumzo ya ana kwa ana na kocha wa Real Madrid Julen Lopetegui huku akilenga kuweka wazi hatma yake katika klabu hiyo. (Sky Sports)

Timu ya Jose Mourinho inajiandaa kuwasilisha ombi la kumnunua beki wa Leicester Harry Maguire, 25, lakini inakabiliwa na changamoto ya kulazimika kulipa dau la £50m kumpata mchezaji huyo wa Uingereza. (Mail)

Eintracht Frankfurt italazimika kusikiza wito wa ombi la Ante Rebic, kulingana na mkurugenzi wa michezo Fredi Bobic. Winga huyo, 24, amehusishwa na Manchester United . (Sport 1 - via Metro)

​​Leicester City imeanza kumnyatia winga wa zamani wa Tottenham Iago Falque, 28, katika harakati za kutafuta winga mpya baada ya kuondoka kwa Riyad Mahrez. (Tutosport - via 90min)

Mchezaji anayelengwa na West Ham Felipe Anderson, 25, amesafiri hadi mjini London huku kiungo huyo wa Brazil akikaribia kuweka rekodi ya uhamisho ya dau la £50m kutoka Lazio. (Sun)

Tottenham huenda ikakosa kumsaini kiungo wa kati wa PSG Adrien Rabiot baada ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 kuwa na hamu ya kujiunga na Barcelona. (Sport - via Football London)

Fulham imejiunga na Wolves katika kujaribu kumsaini winga wa nyuma wa Manchester City na Ukraine Oleksandr Zinchenko, ambaye huenda akagharimu £16m. (Telegraph)

Southampton italazimika kushindana na Lazio katika usajili wa mshambuliaji wa Atalanta Andrea Petagna, 23. (Calciomercato)

Crystal Palace inamnyatia winga wa West Ham Michail Antonio na inajiandaa kuwasilisha dau la £15m. (Sky Sports)

West Ham na Manchester United wameonyesha hamu ya kumsaini beki wa kulia wa Sporting Cristiano Piccini, 25. (Turkish Football)

Southampton inajiandaa kumtoa kwa mkopo beki wake Fraser Forster, 30, baada ya kukamilisha usajili wa kipa kijana Angus Gunn, 22. (Daily Echo)

Everton inamsaka mchezaji wa Barcelona Lucas Digne, 24, pamoja na mchezaji mwenza Yerry Mina, 23. (Mirror)

Beki wa Everton Tyias Browning, 24, anataka kuhamia katika klabu nyengine kwa mkopo baaada ya kuichezea Sunderland msimu uliokwisha . (Liverpool Echo)

​​Kiungo wa kati wa Stoke City Badou Ndiaye ameiambia klabu hiyo kwamba anataka kuondoka msimu huu ili kujiunga tena na klabu ya Galatasaray. (Milliyet - via 90min)

Mkufunzi wa Burnley Sean Dyche anasema kuwa klabu hiyo itavunja rekodi yake ya uhamisho msimu huu . (Lancashire Telegraph)