Johnson & Johnson: Wanawake walioathiriwa na poda ya talc kulipwa $4.7bn Marekani

Johnson & Johnson baby powder

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Johnson & Johnson imesema poda yake imethibitishwa kuwa salama kutokana na utafiti wa miaka mingi

Kampuni ya Johnsons & Johnsons imeamriwa kulipa fidia ya dola za Kimarekani bilioni 4.7 kama fidia na faini kwa wanawake 22 waliodai kuwa bidhaa za talc za kampuni hiyo zimewasababishia saratani ya ovari.

Baraza la Mahakama Missouri huko Marekani limeamuru walipwe dola za kimarekani milioni 550 kama fidia na wakaongeza dola bilioni 4.1 kama adhabu ya fidia.

Uamuzi huo unakuja wakati ambapo kampuni hiyo kubwa ya dawa ikipambana na kesi 9,000 zinazohusisha bidhaa yake maarufu ya poda.

J&J inasema imesikitishwa sana na ina mpango wa kukata rufaa.

Katika kesi hiyo iliyodumu wiki sita, wanawake hao na familia zao wamesema kuwa wamepata saratani ya ovari baada ya kutumia poda ya Johnsons na baadhi ya bidhaa zake za talc kwa miongo kadhaa.

Mawakili wa familia hizo wanasema kuwa kampuni ya Johnsons ilikuwa inatambua kuwa bidhaa yao ya poda ya talc ilikuwa na madini mabaya ya 'asbestos' tangu mwaka 1970 lakini ilikosa kuwaonya watumiaji kuhusu athari.

Kampuni hiyo ilikana kuwa bidhaa zake zimewahi kuwa na madini mabaya ya asbestos na walisisitiza kwamba bidhaa hizo hazileti saratani.

Kampuni hiyo kubwa ya dawa iliongeza kwamba tafiti mbali mbali zimeonyesha kuwa poda yao ni salama na wakasisitiza zaidi kuwa uamuzi huo ni matokeo ya uamuzi usiotenda haki.

Uamuzi uliovunja rekodi

Malipo hayo ndiyo ya juu zaidi kwa J&J kuwahi kuamriwa kulipa kama fidia kutokana na bidhaa zake na tuhuma kwamba huwa zinasababisha kansa.

Katika kesi iliyopita mwaka 2017 jopo la mahakama Calfonia liliiamuru kampuni hiyo kulipa tozo ya dola za kimarekani 417 kwa mwanamke ambaye alisema amepata saratani ya mayai ya uzazi baadha ya kutumia bidhaa za kampuni hiyo ikiwemo poda yake ya watoto (Johnsons baby powdwer)

Hata hivyo baadaye hakimu alibadiliuamuzi huo japo bado kampuni hiyo ina kesi kadhaa ambazo bado hazijatolewa uamuzi.

Adhabu za kulipa fidia mara nyingi huwa zinapunguzwa kwa hakimunwa kesi hiyo au kukata rufaa, na J&J imefanikiwa kubadili maamuzi ya kesi kadhaa huku baadhi ya hukumu hizo wakitoa vigezo vya matatizo ya kiufundi.

Poda ya Talc ni salama?

Uchambuzi wa James Gallagher, mhariri wa afya, mtandao wa habari wa BBC

Kumekuwa na wasiwasi kwa miaka kadhaa kwamba kutumia poda yenye madini ya talcum, hasa kwenye viungo vya uzazi, inaweza kuongeza hatari ya saratani ya ovari. Lakini ushahidi hauja kamilika. Shirika la kimataifa kwa ajili ya utafiti juu ya saratani imeiweka talc inayotumika katika viungo vya uzazi kama madini yenye utata kwasababu ya ushahidi mkanganyiko.

Kwa nini kuna mjadala huu?

Madini ya talc kwa asili yake yana asbestos na yanasababisha saratani, ijapokuwa talc isiyo ya asbestos imekuwa ikitumiwa katika poda za watoto na vipodozi vingine tangu mwaka 1970. Lakini tafiti za matumizi ya madini ya talc yasiyo na asbestos zimekuwa zikitoa majibu yanayo kinzana.

Katika baadhi ya tafiti ilibainishwa kuna hatari ya saratani, ila kuna wasiwasi kuwa tafiti zinaweza onyesha upendeleo kwani zinategemea watu kukumbuka wametumia talc kwa kiasi gani kwa miaka iliyopita.

Tafiti zingine zinasema hakuna mahusiano kabisa. Lakini pia hakuna uthibitisho wa kiasi kinachotumika cha talc ambapo ni tofauti na tumbaku ambayo kadiri unavyozidi kuvuta ndivyo unavyoongeza hatari kubwa ya kupata saratani.