Rais Isaias Afwerki afanya ziara ya kihistoria nchini Ethiopia

Bwana Afwerki aliwasili nchini Ethiopia siku ya Jumamosi -ikiwa ziara yake ya kwanza nchini humo baada ya miongo miwili. Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Bwana Afwerki aliwasili nchini Ethiopia siku ya Jumamosi -ikiwa ziara yake ya kwanza nchini humo baada ya miongo miwili.

Rais wa Eritrea Isaias Afwerki anazuru nchini Ethiopia kwa mara ya kwanza tangu kuanza kwa vita vya mpakani kati ya mataifa hayo mawli 1998.

Ziara hiyo ya siku tatu inalenga kuimarisha uhusiano wao siku kadhaa baada ya viongozi hao kumaliza uhasama wa kivita uliopo kati ya mataifa hayo mawili.

Bwana Afwerki alikaribishwa na waziri mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed alipowasili katika uwnaja wa ndege.

Maelfu ya watu , wengi wakipeperusha bendera za Eritrea, walijipanga kandakando ya barabara za mji mkuu wa Ethiopia Addis Ababa kuadhimisha ziara hiyo ya kihistoria siku ya Jumamosi.

Bwana Afwerki ambaye ziara yake ndio ya hivi karibuni katika harakati za kuleta maridhiano kati ya mahasimu wawili wa Afrika alikaribishwa na wachezaji densi wa Ethiopia huku bandi ikipiga ngoma kumkaribisha alipokuwa akitembea juu ya zulia jekundu.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Wacheza densi wa Ethiopia wanajiandaa kumchezea densi bwana Afwerki akiwasili mjini Adis Ababa
Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Waendesha farasi wa Ethiopia pia walihudhuria hafla hiyo ya kumaribisha rais huyo wa Eritrea

Katika barabara kuu kutoka uwnaja wa ndege , maelfu ya raia wa Ethiopia walikongamana kusherehekea kwa kubeba bendera zote za Eritrea na Ethiopia

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption watu walijipanga kandokando ya barabara People lined roads in Addis Ababa wearing T-shirts emblazoned with images of both leaders

Wiki iliopita bwana Abiy alisafiri hadi mji mkuu wa Eritrea Asmara , ambapo viongozi hao wawili walitia saini makubaliano ya kusitisha mzozo huo huku wakikubaliana kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia baada ya miongo miwili ya uhasama.

Tangu achukue mamlaka nchini Ethiopia mnamo Aprili mosi, bwana Abiy ametangaza msururu wa mabadiliko na kuzungumza kuhusu kuimarisha uhusiano na Eritrea.

Kwa nini makubaliano hayo ni muhimu?

Mataifa hayo mawili yamekuwa katika hali ya 'bila vita hakuna amani' tangu mwaka 2000 wakati makubaliano ya amani yalimaliza vita ambavyo maelfu ya makumi ya raia walifariki.

Tume ya mpakani iliowekwa chini ya makubaliano ya amani iliamuru kwamba mji wa Badme, eneo tata la mgogoro huo linamilikiwa na Eritrea, lakini Ethiopia ilikataa kukubali hilo hivyobasi uhusiano wa kawaida haukuendelea.

Uhasama huo uliathiri eneo zima.

Mataifa hayo yalichukua pande pinzani katika mgogoro wa muda mrefu wa Somalia - huku Eritrea ikilaumiwa kwa kundi la wapiganaji la Al-shabab nayo Ethiopia , mshirika mkuu wa Marekani akiunga mkono serikali ilio madarakani ya Somali.

Hadi kufikia sasa , Eritrea imesema kuwa vita vinaweza uanza upya na hii ndio sababu ina usajili wa kitaifa, au huduma ya kijeshi ya lazima, ambayo inaweza kudumu milele.

Ndio sababu kwamba raia wengi wa taifa hilo wamekuwa wakijaribu kuondoka na kutafuta hifadhi Ulaya

Ziara ya Bwana Afwerki ni ufanisi mkubwa kwa kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 72 ambaye amewtengwa kidiplomasia na anayeonekana kuwa mwenye siri kubwa na anayeonekana kuwa mgonjwa

Kwa nini hili linatokea sasa?

Mbali na kuomba ushirikiano mzuri na Eritrea, bwana Abiy ameondoa hali ya tahadhari , akawafungua wafungwa wa kisiasa na kutangaza mabadiliko ya kiuchumi.

Alirithi taifa ambalo limekuwa na ukuaji mkubwa wa kiuchumi katika siku za hivi karibuni duniani lakini pia taifa ambalo limekuwa likigawanywa na watu ambao wanahisi kutengwa.

Haki miliki ya picha Mela Gebre Medhin
Image caption Jubilant Eritreans took to the streets of the capital, Asmara, last week as Ethiopia's prime minister visited

Serikali ya awali ilikuwa ikishutumiwa kwa kukiuka haki za kibinaadamu -ikiwemo ukatili na mauaji ya wapinzani wa serikali.

Bwana Abiy ni kiongozi wa kwanza wa kabila la Oromo -kabila ambalo limekua likiongoza maandamano dhidi ya serikali kwa miaka mitatu ambayo yamesababisha vifo vya mamia ya watu.

Nini kitakachobadilika?

Mbali na uhusiano wa kidiplomsia na ule wa kibiashara , uchukuzi na mahusiano ya simu yataimarishwa.

Ndege ya kwanza kati ya mataifa hayo mawili baada ya miongo miwili itaanza kusafiri wiki ijayo-huku ikiwa tatizo la kusafiri moja kwa moja kutoka taifa moja hadi jingine kwa kipindi cha miaka 20 iliopita.

Hii inaleta matumaini kwamba familia ambazo zilikuwa zimegawanywa na uhasama huo huenda zikaungana tena.

Haki miliki ya picha Addisalem Hadigu
Image caption Mwandishi wa Ethiopia Addisalem Hadigu anatumai kumuona mwanwae wa kike kwa mara ya kwanza baada ya miaka 16

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii