Vijana wa Thailand wamkumbuka shujaa aliyeshiriki kuokolewa kwao

Watoto 12 na Kocha wao wakiwa na picha ya shujaa Saman Gunan Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Watoto 12 na Kocha wao wakiwa na picha ya shujaa Saman Gunan

Wacheza mpira wadogo 12 waliookolewa kutoka kwenye pango nchini Thailand wanaomboleza kifo cha afisa wa zamani wa kikosi cha askari wa maji aliyepoteza maisha kwenye operesheni ya uokoaji

mpiga mbizi wa kujitolea Saman Gunan alipoteza maisha tarehe 6 mwezi Julai alipokuwa akipeleka mitungi ya gesi ya oksijeni ndani ya pango.

Tangu wakati huo alitambulika kuwa shujaa duniani

''Wote walilia wakitoa salamu zao za rambirambi kwa kuandika ujumbe kwenye picha ya kuchora ya Luteni kamanda Saman na kunyamaza kimya kwa dakika moja kwa ajili yake'', alisema waziri wa afya Jedsada Chokdamrongsuk.

Picha zilionyesha timu ya Wild Boars ambao wanaangaliwa afya zao hospitalini, walikusanyika kuzunguka picha ya mpigambizi.

''Walimshukuru na kumuahidi kuwa watakuwa watoto waziri'', ilisema wizara ya afya.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Vijana wakiwa wameinamisha vichwa baada ya kuandika ujumbe kwenye picha ya shujaa Saman

Wavulana hao wenye umri wa kati ya miaka11-16, walitolewa kutoka kwenye pango na askari wa majini na wataalamu wa kupiga mbizi, operesheni iliyodumu kwa siku tatu, iliyoisha tarehe 10 mwezi Julai.

Wanatarajiwa kuondoka hospitali ya Chiang Rai Prachanukroh siku ya Alhamisi, ingawa wengi bado wanapata dawa za kupambana na vijidudu.

Watatazamwa kwa karibu kuona kama kuna dalili zozote za msongo, dalili ambazo zinaweza kujitokeza miezi kadhaa ijayo.Watoto wamepatiwa ushauri kuepuka kufanya mahojiano na vyombo vya habari, hali ambayo inaweza kuwasababishia hali ya kiwewe.

vijana hao na kocha wao wamealikwa kwenye mchezo wa fainali za kome la dunia 2018 lakini ilishindikana kwa sababu za kitabibu.

Walitumia siku tisa kwenye pango wakiwa na chakula kidogo na mwanga mdogo mapaka walipofikiwa na waokoaji Jumatatu tarehe 2.

waokoaji takriban 100 waliungana kuwafikia na kuhakikisha wanawanasua kutoka pangoni.

Wavulana wote na kocha wao waliokwama pangoni Thailand waokolewa

Picha za kwanza za hospitali za vijana waliokwama mapangoni Thailand zatolewa

Mjane wa Saman ameiambia BBC :''Amesifiwa kuwa shujaa kwa sababu alivyo .Alipenda kuwasaidia wengine na kufanya kazi za kujitoa''.

Watu 4,000 wamejitolea kufanya usafi katika eneo kuzunguka pango baada ya kuharibiwa na shughuli za uokoaji

Maafisa wamesema eneo hilo litafunguliwa tena na kuwa kivutio cha utalii, safari hii likilindwa kwa tahadhari kuepuka kutokea kwa tukio hatari kama mkasa wa vijana hao wadogo.

Mada zinazohusiana