Aliyekuwa mlinzi wa Osama Bin Laden afukuzwa kutoka Ujerumani

Bin Laden file pic from 2011
Maelezo ya picha,

Baada ya shambuliazi la 9/11 Bin Laden alikuwa adui namba moja wa Marekani

Ujerumani imemfukuza mwanamume raia wa Tunisia ambaye wakati mmoja alidaiwa kuwa mlinzi wa Osama Bin Laden na amekuwa akiishi nchini Ujerumani na familia yake tangu mwaka 1997.

Mwanamume huyo mwenye miaka 42 ambaye pia anajulikana kama Sami A aliwekwa kwenye ndege kutoka mji Düsseldorf mapema Ijumaa licha ya mahakama kuagiza asifukuzwe.

Uamuzi wa mahakama ulizifikia mamlaka ukiwa umechelewa sana kuweza kuzuia kufukuzwa kwa Sam A kulingana na maafisa wa mahakama.

Sami A alikuwa amedai kuwa anaweza kuteswa ikiwa angerudishwa Tunisia.

Alikamatwa mwezi uliopita badaa ya mamlaka za uhamiaji kuamua kuwa angefukuzwa. Lakini mahakama ya Gelsenkirchen ilikuwa imetoa uamuzi kuwa hatua hiyo isichukuliwe.

Bin Laden aliongoz amtandao wa al-Qaeda na aligzua mashmabualia mabaya ya Septeman 11 mwalka 2001. Aliuawa na vikosi maalum vya Marekani nchini Pakistan mwaka 2011.

Sami A alionekena kama tisho kwa usalama wakati akiishi mji ulio mashariki mwa Ujerumani wa Bochum, ambapo alikuwa akilipwa euro 1,168 kila mwezi kama msaada. Maombi yake ya kutaka apewe hifadhi mwaka 2007 yalikatawaliwa.

Vyombo vya habari havijataja jina lake kamili kwa sababu za kiusalama.

Amekana kuwa na uhusiano na makundi ya Jihad. Amekuwa akiishi huko Bochum na mkewe mjerumani na watoto wanne.

Takriban marubani watatua kati yale waliohusika na shambulizi la Septemba 11 walikuwa ni wanachama wa kikundi cha al-Qaeda kilichokuwa na makao yake huko Hamburg kaskazini mwa Ujerumani.

Sami A alichunguzwa baada ya kudaiwa kuwa na uhusiano na al-Qaeda mwaka 2006 lakini hakushtakiwa.