Cate Waruguru: Mbunge azuiwa kuingia hotelini Kenya kwa sababu ya cheti cha ndoa

Mwakilishi wa wanawake wa kaunti ya Laikipia, jimbo linalopatikana takriban 250km kaskazini mwa jiji la Nairobi, Bi Catherine Waruguru anasema haki zake za kimsingi zilikiukwa baada yake na mumewe kuzuiwa kuingia katika hoteli moja nchini humo kwa kukosa cheti cha ndoa.

Mbunge huyo ametishia kuishtaki hoteli hiyo ya mjini Kericho, eneo la Bonde la Ufa akisema alidhalilishwa.

Hoteli hiyo imeweka ilani kwamba mwanamume na mwanamke hawawezi kuruhusiwa katika chumba kimoja iwapo hawajaoana.

Lakini mbunge huyo anasema wanandoa wengine waliruhusiwa kuingia bila kuitishwa cheti cha ndoa, na kwamba walifanya kila juhudi kuthibitisha kwamba walikuwa mume na mke ingawa hawakuwa na cheti cha ndoa.

Mwandishi wetu Ane Ngugi amezungumza na mbunge huyo.