Freeman Mbowe: Chanzo cha wabunge 20 wa upinzani kukamatwa Tanzania ni uchaguzi mdogo

Chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania Chadema kimesema wanachama wake 20 akiwemo mbunge walikamatwa siku ya Jumamosi kusini mwa nchi kwa madai ya kusababisha vurugu.

Kamatakamata hiyo, inatokea wakati vyama vya kisiasa vikijiandaa na uchaguzi wa manispaa huko Tunduma kusini mwa Tanzania unaotarajiwa kufanyika mwezi Agosti mwaka huu.

Tumezungumza na kiongozi wa upinzani nchini Tanzania Freeman Mbowe.