Mambo makuu kutoka kwa mkutano wa Trump na Putin

Mambo makuu kutoka kwa mkutano wa Trump na Putin
Maelezo ya picha,

Mambo makuu kutoka kwa mkutano wa Trump na Putin

Mkutano wa Helsiniki kati Vladimir Putin na Donald Trump ulimalizika, baada ya karibu saa mbili faraghani na saa nyingine moja na waandishi wa habari, kuna mambo kadhaa ya kuangaliwa.

Kabla ya kufanyika mkutano huo wanademokrat walimuonya Trump wakimtaka awe mwangalifu dhidi ya Putin huku wengine wakisema kuwa haukuwa uamuzi mzuri kwa Rais wa Marekani kufanya mkutano wa aina hiyo kufuatia madai kuwa maafisa wa jeshi la Uruis wameshtakiwa na kuendesha vita vya mitandao dhidi ya Marekani wakati wa uchaguzi wa mwaka 2016.

Lakini mambo yalionekana kuwa tofauti na haya ni baadhi ya masuala muhimu kutoka kwa mkutano huo.

Sote tunalaumiwa

Bw Trump kwenye swali lake la kwanza kutoka kwa mwandishi wa habari raia wa Marekani, ambapo alitakiwa kueleza baada ya kuandika mapema kwenye mtandao wa twitter kuwa Marekani inalaumiwa kwa hali tete ya sasa kati ya Marekani na Urusi.

Akijibu alishikilia msimamo wa matamshi yake ya awali kuwa anazilaumu nchi zote mbili.

Alisema pande zote zilifanya makosa lakini akakataa kugusia mambo kadhaa yakiwemo kuhusika kwa jeshi la Urusi nchini Ukraine na kulimega eneo la Crimea, shambulizi la kutumiwa kemikali ya Novichok kusini mwa England na kushtakiwa kwa raia wa Urusi kwa kuingilia kati uchaguzi wa Marekani.

Maelezo ya picha,

Mambo makuu kutoka kwa mkutano waTrump na Putin

Badala yake alisisitiza kuwa hakukuwa na ushirikiano kwa njia yoyote ile kati ya timu yake ya kampeni na Urusi.

Alipoulizwa ikiwa anaweza kuishutumu Urusi na Putin moja kwa moja kwa kuingailia kati uchaguzi, Bw Trump alisema maafisa wake wa ujasusi, akiwemo mkurugenzi Dan Coats wamemuambia kuwa wanafikiri kuwa ni Urusi, aliendelea kusema kuwa Putin alimwambia Urusi haukuhusika.

Ghadhabu na kukosolewa

Sio jambo la kushangaza kuwa kile alichokifanya Trumpkilikosolewa vikali. Kiongozi wa wachache katika bunge la Senate Chuck Schumer aliitaja hatua ya Trump kuwa ya aibua ambayo ilikuwa hatari na dhaifu.

John Brennam mkurugenzi wa CIA wakati wa uongozi wa Barack Obama alisema Trump alifanya makosa ya uhaini.

Mgombea urais kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2008 nchini Marekani John McCain alisema alichokifanya Trump kilikuwa kitendo kibaya zaidi kuwai kufanywa na Rais wa Marekani.

Hatua ya kwanza kubwa

Kwa wafuasi wake Trump mkutano huo ni mwanzoa wa jitihada kubwa za kuboresha uhusiano kati ya mataifa makubwa ya nyuklia duniani.

Putin naye alisema mkutano huo ni hatua ya kwanza muhimu.

Bila ya kuwepo matokeo mema kutoka kwa mkutano huo viongozi wote wanauona kuwa mwanzo wa mikutano mingine mingi itakayofuatia.

Hata hivyo kutokana na jinsi mkutano huo umezungumziwa kutoka pande zote za siasa hatma ya mikutano ya baadaye itakuwa muhimu hata kufanyika.,