Kwa Picha: Ndani ya ubalozi wa Eritrea nchini Ethiopia uliofungwa miaka 20 iliyopita

Inside the Eritrean embassy. This and other embassy furniture from twenty years ago has been handed over by the Eritrean leader to his Ethiopian counterpart.
Maelezo ya picha,

Fanicha hii ilitumiwa na balozi wa Eritrea nchini Ethiopia miongo miwili iliyopita

Vyombo vya nyumbani vikwemo fanicha, magari na hata chupa za mvinyo vimefichuliwa wakati Eritrea ilifungua rasmi milango ya ubalozi wake, mjini Addis Ababa kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1998 wakati nchi hizo mbili ziliingia vitani.

Ni sehemu ya mikakati ya kuboresha uhusiano kati ya nchi hizo mbili ambazo hivi majuzi zilikubaliana kuwa na uhusiano wa kidiplomasia licha ya mzozo kumalizika mwaka 2000.

Picha hizi zilinaswa na BBC ndani ya ubalozi.

Maelezo ya picha,

Magari haya yako kwenye ubalozi mjini Addis Ababa

Maelezo ya picha,

Their vintage is unknown but these untouched bottles of wine, beer and olive oil were found in a dusty crate.

Maelezo ya picha,

Rais Isaias Afwerki - akiwa na waziri mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed - akipandisha bendera ndani ya ubalozi kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka 20

Maelezo ya picha,

Isaias (kushoto) na waziri mkuu Abiy (kulia) wakiwa kwenye majengo ya ubalozi

Maelezo ya picha,

Makaazi ya wafanyakajazi wa ubalozi yakiwa na picha ambazo hazijulikani ni za nani

Maelezo ya picha,

Waziri mkuu wa Ethiopia Abiy (katikati) akimpa funguo za ubalozi rais wa Eritrea Isaias (kulia)

Maelezo ya picha,

Bendi wakati wa kufunguliwa kwa ubalozi mjini Addis Ababa

All pictures subject to copyright.