Mataifa 5 ya Afrika yaliowahi kubadilisha jina.

Kiongozi wa upinzani Zimbabwe Nelson Chamisa ameapa kuwa atalibadilisha jina la nchi ya Zimbabwe
Maelezo ya picha,

Kiongozi wa upinzani Zimbabwe Nelson Chamisa ameapa kuwa atalibadilisha jina la nchi ya Zimbabwe

Kiongozi wa upinzani Zimbabwe Nelson Chamisa ameapa kuwa atalibadilisha jina la nchi hiyo na kuwa "Great Zimbabwe" akieleza kuwa jina la sasa la nchi hiyo lina 'laana', kwa mujibu wa mtandao wa New Zimbabwe.

"Zimbabwe haiwezi kusalia kuwa Zimbabwe, kwasababu imegeuzwa kuwa gofu la Zimbabwe," Chamisa aliwaambia maelfu ya wafuasi katika mkutano wa kisiasa mashariki mwa mji wa Mutare.

"Jina la Zimbabwe limelaaniwa kama mnavyoona timu yetu ya taifa ya soka inashindwa kila saa katika mechi - kriketi tunashindwa, voliboli daima inashindwa," aliongeza kusema.

Kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 40 ananuia kuwa rais katika uchaguzi mwishoni mwa mwei huu Julai 30 - uchaguzi ulio wa kwanza baada ya kiongozi wa muda mrefu Robert Mugabe kuondoka madarakani.

Lakini hii sio mara ya kwanza kwa Zimbabwe kubadili jina la nchi.

Zimbabwe ilijulikana kama Rhodesia kusini kati ya mwaka 1898-1964, ambalo ni jina la Mkoloni wa Uingereza Cecil Rhodes. Mapema 1960, however, raia wenye utaifa walianza kuliita taifa hilo Zimbabwe. Jina linalotokan ana maneno mawili "dzimba" na "dzamabwe" (yenye maana ya nyumba ya mawe) kwa lugha ya Shona inayozungumzwa pakubwa hivi leo Zimbabwe.

Je ni ngani nyingine za Afrika zilizowahi kubadili jina?

Maelezo ya picha,

Rais Thomas Sankara, alilipa taifa hilo jina rasmi la Burkina Faso mnamo August 1984 kutoka jina lillilokuwepo Upper Volta

Burkina Faso:

Rais Thomas Sankara, kiongozi mshupavu na kijana wa iliyokuwa inajulikana kama Upper Volta, alilipa taifa hilo jina rasmi la Burkina Faso mnamo August 1984.

Alilichagua jina hilo ambayo ni maneno mawili "Burkina" na "Faso" kutoka makabila mawili makuu yanayozungumzwa nchini.

Jina la zamani la Upper Volta lilitoka kwa Ufaransa iliyokuwa mkoloni kutokana na mto wa Voltauliopita katika eneo hilo.

Burkina katika lugha ya Mòoré lina maana "wanaume wenye heshima" na Faso katika lugha ya Dioula lina maana "alikozaliwa baba"; yakichanganywa, Burkina Faso lina maana "eneo la watu wa kweli."

Maelezo ya picha,

Julius Nyerere alikuwa na ushawishi mkubwa katika mataifa ya Afrika kujipatia uhuru.

Tanzania:

Tanganyika ndio jina la eneo lililokuwa huru kati ya maziwa makuu ya Afrika na Bahari Hindi lililokuwepo kuanzia 1961, lilipopata uhuru kutoka Jumuiya ya Madola.

Kati ya 1962 na 1964 taifa hilo lilijiita Jamhuri ya Tanganyika.

Zanzibar ya zamani, kwa upande mwingine ilijumuisha visiwa vidogo katika bahari Hindi.

Mnamo April 1964, Zanzibar iliungana na Jamhuri ya Tanganyika kuunda Jamhuri ya watu wa Tanganyika na Zanzibar.

Mnamo 1965, Jamhuri hiyo iliunganisha majina ya nchi hizo mbili na kuwa: Tanzania.

Maelezo ya picha,

Kwame Nkrumah nchini Ghana

Ghana:

Ghana ililibadilisha jina lake kutoka Gold Coast mnamo 1957 kuendana na hadhi yake mpya ya kuwa Jamhuri baada ya kujinyakulia uhuru kutoka kwa Mkoloni Muingereza.

Kiongozi wa kwanza wa Ghana Dr. Kwame Nkrumah alilipa taifa hilo jina jipya muda mfupi baada ya kujinyakulia uhuru.

Na jina hilo linaaminika kutokana na majina ya Wafalme wa jadi (Gana) wa ufalme wa Wagadugu uliolitawala eneo linalojulikana leo kama Ghana.

Jamhuri ya Benin:

Dahomey ndio lililokuwa jina la ufalme uliokuwepo Afrika magharibi ambao leo unajulikana kama Jamhuri ya Benin.

Kwa wakati mmoja ufalme wa Dahomey ulisambaa hadi katika zinazojulikana leo kama Benin, Togo, na sehemu kadhaa za kusini maharibi mwa Nigeria.

Dahomey ulikuwa maarufu kwa mashujaa wake wa kike waliokuwa na uweledi wa kupigana vita na kwa mara nyingi walitumika kama walinzi wa ufalme.

Mnamo 1975, chini ya uongozi wa Mathieu Kerekou, Dahomey ilibadilishwa jina na kuwa Jamhuri ya Benin.

DRC:

Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo DRC ilikuwa ikifahamika kama Leopoldville katika karne ya 19 ilipokuwa chini ya ukoloni wa ufalme wa Ubelgiji.

Kati ya 1908 na 1960, ilifahamika kama Belgian Congo.

Hatahivyo wakati taifa hilo lilipojipatia uhuru mnamo 1960, viongozi wake walilibadili jina na kuwa Congo kutoakana na mto Congo unaopita katika sehemu nyingi za nchi hiyo.

Mnamo 1971, rais Mobutu Sese Seko kwa mara nyingine alilibadili jina, na kwa mara hii akaliita taifa hilo Jamhuri ya Zaire.

Baada ya kiongozi huyo kutimuliwa mnamo 1996 na serikali mpya ya Laurent Kabila kuingia madarakani mnamo 2007 nchi hiyo ilipewa jina lake la zamani.