Rais Nicolas Maduro wa Venezuela asema Afrika ilishinda kombe la Dunia

Rais Nicolas maduro wa Venezuela
Maelezo ya picha,

Rais Nicolas Maduro wa Venezuela asema Afrika ilishinda kombe la Dunia

Afrika iliishindia Ufaransa kombe la Dunia , na Ulaya inafaa kusitisha ubaguzi dhidi ya wahamiaji kulingana na rais wa Venezuela Nicolas Maduro.

Akizungumza katika mji mkuu wa Caracas, chombo cha habari cha kitaifa kilimnukuu akisema.

Maelezo ya picha,

Paul Pogba asherehekea na wenzake baada ya kufunga bao katika kombe la dunia

''Timu ya Ufaransa ilishinda ijapokuwa ilikuwa kama ya Afrika . Ukweli ni kwamba Afrika ilishinda-wahamiaji wa Afrika waliowasili nchini Ufaransa, natumai Ulaya itapokea ujumbe huo''.

''Ulaya haifai kuwabagua Waafrika, hakuna ubaguzi dhidi ya wahamiaji. Ufaransa iliishinda Croatia 4-2''.

Ruka Twitter ujumbe, 1

Mwisho wa Twitter ujumbe, 1

Timu hiyo ilikuwa na mchangnyiko mkubwa wa rangi katika michuano hiyo- wachezaji 15 kati ya 23 waliopo katika kikosi cha kitaifa wana mizizi yao Afrika ,hususan kutoka mataifa yaliotawaliwa na Ufaransa.

Maelezo ya picha,

Ndio mchezaji mwenye umri mdogo tangu Pelle kufunga katika kombe la dunia , wazazi wake wanatoka cameroon na Algeria

Matamshi yaliotaja kikosi hicho cha Ufaransa yamezua mjadala katika mitandao ya kijamii kuhusu ubaguzi wa rangi na uhamiaji.

Muda mfupi baada ya Ufaransa kuilaza Croatia siku ya Jumapili Khaled Baydoun mwandishi wa Marekani kuhusu vita dhidi ya Uislamu alitaka kuwepo kwa haki kwa timu hiyo.

Chapisho hilo limesambazwa zaidi ya mara 163,000 na kupendwa mara 370,000 tangu lilipochapishwa siku ya Jumapili kufuatia ushindi wa Ufaransa wa 4-2.

Wengi katika mitandao ya kijamii walisema kuwa licha ya mizizi ya kutoka Afrika , wanaume hao walikuwa Wafaransa kwanza, huku wengine wakimshutumu Beydoun kwa kutumia michezo kufanya siasa.

Wengine waliamini kwamba chapisho hilo la Twitter litaumiza uhusiano wa rangi katika taifa ambapo swala hilo ni tata kufuatia mgogoro wa hivi karibuni wa wahamiaji pamoja na mashambulio ya kigaidi.

Ruka Twitter ujumbe, 2

Mwisho wa Twitter ujumbe, 2

Mwaka 2016, mwaka mmoja baada ya shambulio baya la kigaidi, mchezaji wa zamani wa Ufaransa Louis Saha alisema kuwa Ufaransa ingali nyuma ya mataifa mengine katika kukabiliana na ugaidi.

Ni mara ya pili Ufaransa imejishindia taji la kombe la dunia. Kabla ya kujishindia taji la 1998 kiongozi wa mrengo wa kulia Jean-Marie Le Pen alikuwa amewakosoa baadhi ya wachezaji wake akiwemo Zinedine Zidane ambaye ana mizizi ya Algeria.

Alikuwa amesema kuwa wengi wao walikuwa wageni ambao walikuwa hawaimbi wimbo wa taifa kabla ya mechi.

Mwaka huu kumekuwa na kimya kikuu kutoka chama cha mrengo wa kulia.

Mchapishaji wa ujumbe huu wa Twitter alisema kuwa anatumai kwamba ushindi wa Ufaransa wa 2018 utasaidia kubadilisha fikra.

Ruka Twitter ujumbe, 3

Mwisho wa Twitter ujumbe, 3