Teknolojia: Kamera zinazotambua iwapo una raha ama wewe ni tishio kwa usalama

Uso wa mwanamke ukisomwa
Maelezo ya picha,

Affectiva inasema kuwa teknolojia yao inaweza kutambua hisia za uso

Teknolojia ya kutambua nyuso inaendelea kuimarika , huku kampuni nyengine zikisema kuwa sasa inaweza kusoma hisia na kutambua tabia zinazotilishaka. lakini hii ina athari gani kwa uhuru wa faragha na ule wa kiraia?

Teknolojia hiyo ya kutambua sura imekuwepo kwa miongo kadhaa sasa, lakini imekuwa ikiimarika polepole katika miaka ya hivi karibuni kutokana na maendeleo katika maono ya kompyuta na mfumo wa mitambo inayoweza kufikiria kama binadamu.

Wataalam wa teknolojia wamesema teknolojia hiyo sasa inatumika kuwatambua watu katika mipaka , kufungua simu aina ya Smartphone, kuwakamata wahalifu na kuelezea waliohusika katika kufanya shughuli za benki.

Lakini kampuni nyengine za teknolojia zinasema kuwa zinaweza kutambua hisia zetu. Tangu 1970, wanasaikolojia wanasema kuwa wamefanikiwa kugundua hisia zilizojificha kwa kusoma hisia katika uso ndani ya picha ama video.

Kamera za kiwango cha juu zinaweza kubaini hilo vizuri na kwa haraka.

Maelezo ya picha,

Simu aina ya iPhone X inaweza kufunguliwa kwa utambuzi wa uso.

"Duka la jumla linaweza kuitumia katika njia zilizopo katikati ya bidhaa zake , sio kutambua watu, lakini kubaini aliyeingia ndani kutokana na umri na jinsia pamoja na hisia zao.

Zinaweza kutumika katika ukuzaji wa bidhaa na uwekaji wa bidhaa mpya. kampuni ya utafiti wa soko kantar Millward Brown inatumia teknolojia iliovumbuliwa na kampuni moja ya Marekani kubaini vile wateja wanavyoitikia matangazo ya runinga.

Affectiva inarekodi kanda za video za nyuso za watu kwa ruhusa yao, na baadaye kuchunguza hisia zao za kwa kutumia fremu za siri ili kubaini hisia zao.

''Sisi huwaoji watu lakini tunawaelewa zaidi kwa kuangalia hisia zao. Unaweza kuona ni eneo gani la tangazo linalofanya vyema na hisi zinazotolewa'' , alisema Graham page, mkurugenzi mkuu katika kampuni ya Kantar Millward Brown.

Maelezo ya picha,

Teknolojia ya WeSee inatumika kutambua hisia za watu wakati wa mahojiano

Cha kuongeza utata ni kwamba kampuni nyengine za teknolojia zinatoa teknolojia ambazo zinaweza kutambua hisia kwa lengo la kuimarisha usalama.,

Kwa mfano kampuni ya Uingereza ya WeSee, inasema kuwa teknolojia yake inayofikiria kama mwanadamu inaweza kugundua tabia zinazotilia shaka kwa kusoma hisia zisizoweza kuonekana na jicho la kawaida.

Hisia kama vile wasiwasi na hasira zinaweza kufichwa ikilinganishwa na lugha inayozungumzwa.

WeSee inasema kuwa imekuwa ikishirikiana na shirika kubwa la kuhimiza sheria kufuatwa kuwachunguza watu wanaofanyiwa mahojiano.

Katika siku zijazo kamera za kanda za video katika kituo cha reli zinaweza kutumika kutambua tabia inayotiliashaka na kuripoti kwa mamlaka kuhusu tishio la kigaidi.

Maelezo ya picha,

Je uchunguzi wa hisia unaweza kuwatambua watu walio na lengo la kusababisha shida katika hafla kubwa

"Utafiti kama huo unaweza kufanyiwa makundi ya watu katika hafla kama vile kandanda ama mikutano ya kisiasa. lakini Bwana Phillipou anatilia shaka uhakiki wa hisia zinazogunduliwa.

Wakati unapotaka kutambua nyuso pekee kuna makosa machache hutokea- kampuni bora zaidi zinadai kwamba zinaweza kutambua watu kwa asilimia 90-92.

''Unapojaribu kuchunguza jinisia makosa makubwa hupatikana''.

Maelezo ya picha,

Maafisa wa polisi wa South Wales huchunguza nyuso za watu kwa kutumia kamera

Wakati watazamaji walipohudhuria hafla ya BBC Radio 1's mjini Swansea mnamo mwezi Mei, wengi hawakujua kwamba sura zao zilikuwa zikichunguzwa ikiwa ni miongoni mwa uchunguzi mkubwa uliofanywa na maafisa wa polisi wa South Wales.

Mtu mmoja ambaye alikuwa akitafutwa aligunduliwa na kukamatwa katika dakika 10 baada ya teknolojia hiyo kuwekwa katika tamasha hilo la muziki, kulingana na Scott lloyd kiongozi wa mradi wa maafisa wa polisi wa South wales

Ruka Twitter ujumbe, 1

Mwisho wa Twitter ujumbe, 1

Lakini kundi la haki za binaadamu Liberty linasema kuwa teknolojia hiyo imepokea majibu yasio sahihi katika michuano kama vile ya vilabu bingwa Ulaya katika uwnaja wa Cardif mwaka uliopita

Na mnamo mwezi Julai, wakaazi wa Cardiff Ed Bridges - wanaowakilishwa na Liberty - walianza kuchukua hatua za kisheria dhidi ya kikosi hicho , wakidai kwamba AFR linakiuka faragha na halichunguzwi , hatua iliosababisha kesi kuwasilishwa mahakamani.

Maelezo ya picha,

Maafisa wa polisi wa China hivi majuzi walianza kuvalia miwani inayoweza kutambua hisia za uso wa watu