Kizza Besigye: Upinzani Afrika usishurutishwe kukubali matokeo kwa kusingizia utulivu

Kiongozi wa upinzani na hasimu mkubwa wa Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni, Bw Kizza Besigye ameyashutumu mataifa ya Magharibi kwa kukandamiza hali ya demokrasia ya mataifa ya Afrika.

Anasema mataifa ya Afrika yanafaa kuachiwa nafasi ya kukuza demokrasia na upinzani haufai kushurutishwa kukubali mambo yalivyo ‘kwa ajili ya amani’ baada ya uchaguzi.

Aidha Bwana Kizza Besigye, amesema kuwa miaka mingi ya Bw Museveni kusalia madarakani, ndiyo chanzo cha utovu wa usalama na mauaji ya watu mashuhuri nchini humo, hasa katika mji mkuu Kampala.

Video: Peter Njoroge, BBC, Mwandishi Anne Ngugi, BBC