Benki Mezani: Mpango wa benki unaowapa wanawake ‘uhuru’ Kenya

Kundi moja la wanawake katika eneo la Mogotio, Baringo katika Bonde la Ufa limekuwa likitumia njia ya kipekee kuwafikishia wanawake huduma za kifedha.

Mfumo huo unaofahamika kama ‘benki ya mezani’ hushirikisha wanawake wanaoungana pamoja na kuweka akiba na kuchukua mikopo kwa riba nafuu.

Wanachama hukopa kwa kiwango cha riba cha 1% kwa kipindi cha miaka mitatu.

Mpango huo huwawezesha wanawake kuanzisha biashara na kuwawezesha kujikimu kimaisha na kukidhi mahitaji ya familia zao bila kuwategemea wanaume kama ilivyo kawaida katika jamii nyingi Afrika.

Baadhi ya wanaume wamevutiwa na mpango huu kiasi cha kuendeleza uanachama wake zao wanapofariki.