Ilikuwaje kijana huyu akapunguza uzani kutoka kilo 237 hadi 165

Akiwa na uzani wa kilo 237 Mihir Jain kutoka Dehli, India alifahamika kama kijana mwenye uzani wa juu zaidi duniani. Akiishi kwa kula pizza na pasta, kijana huyu wa umri wa miaka 14 alilazimika kuacha shule. Lakini baada kula chakula chenye mafuta kidogo na kufanyiwa upasuaji amepoteza thuluthi moja wa uzani wake wa mwili.