Ndege ya abiria ya Ethiopia yafanya safari ya kwanza kwenda Eritrea baada ya miaka 20

Ndege ya abiria ya Ethiopia yafanya safari ya kwanza kwenda Eritrea
Image caption Ndege ya abiria ya Ethiopia yafanya safari ya kwanza kwenda Eritrea

Ndege ya shirika la ndege la Ethiopia iliyo na abiria 465 imeondoka nchini Ethiopia ikiwa safarini kwenda Eritrea ikiwa ndiyo safari ya kwanza ya aina hiyo kwa ya miaka 20.

Kwenye safari hii maafisa wa serikali, wafanyabiashara, waandishi wa habari na wale walio na nia ya kukutana na familia zao zilizotenganishwa kwa zaidi miaka 20 wamesafiri.

Wakati vita vya mpaka vilizuka kati ya Ethiopia na Eritrea mwezi Mei mwaka 1998, shirika la kimataifa la safari za ndege lilifunga anga kati ya Eritrea na Ethiopia.

Image caption Ndege ya abiria ya Ethiopia yafanya safari ya kwanza kwenda Eritrea katika miaka 20

Ndege ya shirika la ndege la Ethiopia ilifanya safari ya mwisho kwenda Asmara tarehe 13 Mei 1998. tangu wakati huo anga kati ya nchi hizo imekuwa haipitiki ndege.

Wakati wa ziara ya siku mbili ya waziri mkuu wa Ethiopia nchini Eritrea wiki iliyopita, nchi hizi mbili zilisaini makubaliano kadhaa yakiwemo ya kufufua usafiri wa angania na ardhini

Shirika la ndege la Ethiopia lilikuwa limeomba wizara ya mashauri ya nchi za kigeni na halmashaui ya safari za ndege kufungua anga kwa safari za kibiashara.

Image caption Ndege ya abiria ya Ethiopia yafanya safari ya kwanza kwenda Eritrea katika miaka 20

Shirika la ndege la Ethiopia lilikuwa linafanya safari kwenda mashariki ya kati na Ulaya kupitia anga ya Eritrea. Wakati vita vilizuka lililazimika kubadilisha njia kupitia nchini Sudan na Djibouti hatua iliyochangia kuongezeka safari na matumzi ya mafuta.

Wakati sasa anga hiyo imefunguliwa, ndege za shirika la Ethiopia zinaweza kutumia njia ya zamanai ambayo itapunguza muda wa kusafiri na matumiza ya mafuta. Mashirika mengine ya kimataifa pia nayo yanaweza kuitumia angani hiyo.

Kutokana na kufungwa kwa anga hiyo waziri mkuu Abiy wakati akifanya ziara nchini Eritrea ndege yake la Boeing 737-800 NG, ililazimika kupitia nchini Djibout.