Kundi la waasi la MRDC latuhumu kupambana na jeshi la Rwanda

Major Callixte Sankara
Image caption Major Callixte Sankara

Mamlaka nchini Rwanda zimetupilia mbali uvumi kuhusu kuwepo ukosefu wa usalama maeneo yanayozunguka msitu wa Nyungwe, ambapo kundi jipya la waasi wa MRCD linalodai kuwa linataka kuangusha uongozi wa Rais Paul Kageme linasemekana kuwa na ngome yake.

Akiongea na wenyeji wa wilaya wa Nyaruguru, inspekta mkuu wa polisi Emmanuel Gasana alisema kuwa licha ya majambazi wachache kuvuka na kuingia Rwanda na kuwapora watu eneo moja la Nyaruguru hali hiyo ilikuwa imeshughulikiwa vilivyo na vikosi vya usalama na majambazi hao kukimbilia eneo walitoka.

Kundi la MRCD (Rwanda Democratic Movement for Change) limetangaza rasmi uasi dhidi ya serikali ya Rwanda. Msemaji wa kundi hilo meja Callixte Sankara ameiambia BBC kwamba ni mwezi mzima sasa tangu majeshi ya kundi lake yakipigana na majeshi ya Rwanda katika msitu wa Nyungwe kusini mwa nchi hiyo ,na kwamba majeshi yao yamehusika katika mashambulizi ya mwezi uliopita katika kijiji cha Nyabimata karibu na msitu huo.

Image caption MRCD linadaiwa kuwa ngome yake kwenye msitu wa Nyungwe

Je, huyu kiongozi wa kundi jipya la waasi Meja Callixte Sankara ni nani?

Na mhariri wa BBC, Wanyama wa Chebusiri

Ni machache yanayojulikana kuhusu Callixte Sankara, mtu aliyejitangaza kama naibu kamanda na msemaji wa kundi jipya la waasi la Rwanda Movement for Democratic Change. Meja Callixte Sankara, kama avyojitambulisha kwa vyombo vya habari, ni Mtutsi ambaye alinusurika maauji ya kimbari ya 1994 nchini Rwanda.

Wazazi wake na jamaa wake wote waliuawa na wanamgambo wa Kihutu- Interahamwe.

Kwa sasa ana umri wa miaka 34. Hakuwahi kuwa mwanajeshi wa RPF kwa kuwa RPF ilishika madaraka akiwa na umri wa kama miaka 10.

Baada ya kuhitimu sheria katika chuo kikuu cha Rwanda- Butare, Callixte Sankara, alizozana na serikali ya Rwanda, akakimbilia Afrika ya kusini ambako alijiunga na NRC- Rwanda National Congress, ambayo ilibuniwa na Kayumba Nyamwasa, jenerali wa zamani katika serikali ya Rwanda.

Baadaye alijitenga na RNC na kuanzisha kundi la RRM, Rwandan Revolutionary Movement.

Hivi karibuni, kundi la RRM lilliungana na kundi PDR Ubuyanja linaloongozwa na Paul Rusesabagina, ambaye alijulikana duniani kwa kuokoa Watutsi na watu wengine waliokuwa wamekimbilia katika hoteli Mille Collines mwaka 1994 na kundi la CNRD -the National Council for the Renewal and Democracy ambalo lina wapiganaji wengi wakimbiizi walioko nchini Congo.

Hilo kundi la CNRD lilijitenga na kundi la wapiganji wa zamani wa Kihutu- FDLR ambalo Rwanda imekuwa ikisema kuwa walihusika na mauaji ya mwaka 1994.Makundi hayo yameunda kundi la muungano linalojiita Rwandan Movement for Democratic Change (MRCD)

Kundi hilo lilimchagua Paul Rusesabagina kama kiongozi wake na Major Callixte Sankara ni makamu wa pili na msemaji wapiganaji FLN.

Kamanda wa FLN ni Jenerali Habimana Amada ambaye ametoka katika kundi la CNRD.

Mada zinazohusiana