Je ni kweli Al shabaab ina mfumo bora wa kutoza kodi?

Alshabaab Haki miliki ya picha AFP

Taasisi moja ya utafiti nchini Somalia imesema kwamba kundi la wapiganaji wenye itikadi kali la Al Shabaab lina mfumo bora wa ulipaji kodi ambao unasababisha kupata mamilioni ya dola kwa mwaka.

Kundi hilo la Alshabaab limekuwa likifanya mashambulizi ya kigaidi na maelfu ya watu kupoteza maisha, na kusababisha uchumi wa Somalia kuzorota, hali ambayo pia imeifanya nchi hiyo kuzalisha wakimbizi maeneo mbalimbali duniani.

Taasisi hiyo ya Hiraal imesema ingawa kundi hilo lenye itikadi kali linafanya shughuli zake tu katika maeneo ya kusini mwa Somalia, hulazimisha watu katika maeneo mengi ya nchi kulipa kodi, ikiwemo katika mji mkuu Mogadishu, ambao unashikiliwa na majeshi ya serikali.

Mkuu wa taasisi ya Hiraal Hussein Sheikh- Ali amesema kwamba wapiganaji hao wenye itikadi kali wamejipatia zaida ya dola za Kimarekani milioni 10 katika kipindi cha mwaka 2016 kutokana na kodi iliyotokana na mifugo.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Soko la Bakara katika mji mkuu Mogadishu

''Al Shabaab kama kundi lingine la wapiganaji na la kigaidi limekuwa likikusanya fedha kutoka vyanzo mbalimbali vya mapato. Lilianza kwa kukusanya mapato kidogo kutoka kwa watu waliokuwa wakiwaunga mkono ndani na nje ya nchi.

''Lakini kundi hilo lilipopanuka na kuwa kubwa walianza kujenga mfumo wao wa ukusanyaji ushuru katika maeneo yote ya Somalia'' anasema Hussein Sheikh-Ali.

Mfumo wa kodi

Al-Shabab linaonekana kuwa na mfumo unaofanya kazi vizuri wa utozaji kodi ambao wachache wanasubutu kuukiuka, kwa mujibu wa gazeti la Marekani Washington Post.

Hili linatajwa kuleta mtiririko wa kipato cha kuimarika.

Mambo matano aliyoyasema Obama katika hotuba ya Mandela

Na zaidi, al-Shabab linaonekana kuwa na kiwango kidogo cha rushwa tofauti na baadhi ya mataifa katika nchi zinzaoendelea.

Pengine hilo ndilo linaloonekana kuufanya mfumo wa kundi hilo kuwa bora.

Taasisi ya Hiraal imesema kwamba wakati baaadhi ya watu na biashara hulipa kwa fedha taslimu, wapiganaji hao wana uwezo wa kupata kiasi cha dola milioni 10 kwa mwaka kutoka kwa watu ambao wanalipa kupitia mifugo yao.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Hiraal imesema wapiganaji wa Alshabaab wana uwezo wa kupata kiasi cha dola milioni 10 kwa mwaka kutoka kwa watu ambao wanalipa kupitia mifugo yao

Mwaka jana serikali ya Somali kwa mara ya kwanza iliwaonya wafanya biashara dhidi ya kulipa kodi kwa Al Shabaab baada ya kuibuka taarifa kuuhusu utozaji huo.

Waziri wa ulinzi Somalia, Mohamed Abukar Dualle aliwaambia waandishi habari,

"Utawawajibisha na kuzifunga biashara za watu wanaolipa kodi kwa al Shabaab. Serikali haitokubali ufadhili kwa kundi hilo," waziri alisema.

Idara hiyo ya ulinzi ilionya kuwa hatua za kisheria zitaidhinishwa dhidi ya watakokiuka maagizo hayo ya serikali.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Alshabaab limepoteza sehemu kubwa ya udhibiti wake kutokana na operesheni ya vikosi vya Umoja wa Afrika AMISOM vinavyolinda amani Somalia

Na onyo hilo lilitolewa katika wakati ambapo kundi wapiganaji hao wa kiislamu wal;ikuwa wamepiga marufuku matumizi ya shilingi ya Somalia katika maenoe ya kati na ya kusini wanayoyadhibiti kutokana na kiolichotajwa kuwa ongezeko la fedha bandia.

Biashara zilisita katika enoe la Hiiraan kufuatia marufuku dhidi ya sarafu hiyo ya pekee inayotumika nchini Somalia.

Rais wa Venezuela: Afrika ilishinda kombe la Dunia

Jina Zimbabwe lina 'laana'

Al Shabaab imetekeleza mashambulio yaliosababisha maafa makubwa licha ya kupoteza sehemu kubwa ya udhibiti wake kutokana na operesheni ya vikosi vya Umoja wa Afrika AMISOM vinavyolinda amani Somalia.

Kundi hilo limekuwa likidai kuwa linataka kuwatimua walinda amani hao, kuipindua serikali ya Somalia inayoungwa mkono na mataifa ya magharibi na kuidhinisha sheria za dini ya kiislamu Somalia.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii