Mfanyakazi azawadiwa gari na mwajiri wake baada ya kutembea umbali wa kilomita 32

Bwana Carr akitokwa na machozi ya furaha baada ya heshima aliyoipata Haki miliki ya picha CBS
Image caption Bwana Carr akitokwa na machozi ya furaha baada ya heshima aliyoipata

Mmiliki wa Kampuni moja nchini Marekani amempatia mfanyakazi wake gari mpya baada ya kutembea kwa miguu umbali wa kilomita 32, ambaye alitembea umbali huo usiku mzima akienda kazini

Baada ya gari yake kuharibika, Walter Carr alitembea kwa muda mrefu akipita viunga vya Birmingham, Alabama , mpaka mahali palipo ajira yake mpya.

Afisa wa Polisi alizungumza na Carr akiwa njiani , alivutiwa na moyo aliokuwa nao akamualika kupata kifungua kinywa.

Carr alimwagiwa sifa kedekede mtandaoni tangu habari yake ilipotolewa mitandaoni

Jenny Lamey, mteja wa kampuni hiyo, aliandika kwenye ukurasa wa Facebook kuwa yeye na mumewe waliamka mapemaIjumaa iliyopita kujiandaa tukiwasubiri watu wa Kampuni ya removal iliyokuwa waliokuwa wanawatarajia kuwasili saa mbili kamili.

Ilipotimia saa kumi na mbili na nusu kengele ya mlangoni iliita na bi Lamey alikutana na Bwana Carr ambaye aliongozana na afisa wa polisi kutoka kikosi cha Pelham

''Afisa wa polisi alisema kuwa walikutana njiani asubuhi ile wakanywa chai pamoja, walipofahamu historia yake wakaamua kumleta Walter nyumbani''.

Haki miliki ya picha CBS
Image caption Carr akiwa kwenye gari yake mpya

Bi Lamey alisema kuwa alimruhusu apumzike kabla wafanya kazi wenzake hawajafika nyumbani, lakini Carr alikataa na akaanza kufanya kazi.

Wakati alipokuwa akimsaidia jikoni, alisema , alimweleza hadithi ya rafiki yake wa utotoni wa New Orleans, Louisiana, na jinsi familia yake ilivyohamia Houston,Texas, baada ya nyumba yao kuharibiwa na kimbunga cha Katrina.

''Siwezi kukueleza namna alivyonigusa kutokana na safari yake.''.Alisema Bi Lamey.

''Siwezi kupata picha namna gani alivyosumbuka kutembea usiku mwingi na hakutaka kurudi nyuma.Ni mara ngapi alijiuliza kama hilo lilikuwa wazo zuri''.

''Lakini alitembea mpaka akafika hapa, ninahisi nina deni kwake! aliendelea.

Luke Marklin Mkurugenzi Mkuu alikwenda kwenye kampuni kumuona muajiriwa wake mpya.

Baada ya mazungumzo na kikombe cha kahawa, Marklin alimpatia Carr funguo za gari kwa ajili ya gari yake mpya ya Ford Escape ya mwaka 2014.

Haki miliki ya picha BELLHOPS
Image caption Alionyesha mshangao alipokuwa akipokea zawadi

''Nimefurahishwa sana na aichokifanya, alisema Bwana Marklin.''kila kitu aihokifanya siku ile hakika ndivyo tulivyo-watu weye moyo na shupavu''.

''Akiwa mwenye hisia aliuliza ''Kweli?'', Kisha akamkumbatia Marklina na kupokea funguo za gari.

Kampeni ya mtandaoni kumsaidi bwana Carr kutengeneza gari yake ilisaidia kupatikana kwa dola 8,000 za Marekani.

Carr anatarajiwa kuhitimu mafunzo yake ya shahada yake ya kwanza katika masomo ya afya mwezi Desemba.

''Nilitaka kuwaonyesha kuwa nimebahatika.Nilisema nitaipata kazi hii kwa njia moja au nyingine''.

Aliendelea: ''Ninataka watu wafahamu hili-pamoja na changamoto mbalimbali, ni wewe wa kuweza kupambana zao.Hakuna kisichowezekana isipokuwa tu ukikifanya kisiwezekane.

Bi Lamey alimkumbatia Bwana Carr pia baada ya kupokea zawadi na kumwambia ''Umeyabadili maisha yetu sote Walter''.

''Huwezi kujua umabadili maisha ya watu wangapi na kuwagusa wangapi''.

''Ni mtu wa kipekee sana na utafanya mambo makubwa''.