Zaidi ya wakimbizi 30,000 wanaoishi Tanzania warudi Burundi

Zaidi ya wakimbizi 30,000 wanaoishi Tanzania warudi kwao Burundi
Maelezo ya picha,

Zaidi ya wakimbizi 30,000 wanaoishi Tanzania warudi kwao Burundi

Zaidi ya wakimbizi 30,000 wa Burundi wamerudi nyumbani kutoka kwa kambi zao nchini Tanzania tangu mpango wa wakimbizi hao kurudi nyumbani kwa hiari uanze mapema mwaka huu.

Hatua hii inakuja baada ya mkutano kati ya Rais wa Tanzania John Magufuli na mwenzake rais wa Burundi Pierre Nkurunziza mwezi Julai mwaka uliopita, wakati waliwashauri wakimbzi hao kurudi kwao.

Maelezo ya picha,

Zaidi ya wakimbizi 30,000 wanaoishi Tanzania warudi kwao Burundi

Wito huo mara moja ulianza kukosolewa kutoka kwa makundi wa kutetea haki kwa sababu bado kuna ripoti za ukiukaji wa haki za binadamu nchini Burundi.

Zaidi ya watu 310,000 raia wa Burundi walikimbia nchi yao mwaka 2015 baada ya Burundi kutumbukia kwenye mzozo wakati Rais Pierre Nkurunziza, alishinda uchaguzi kwenye muhula wa tatu uliokumbwa na utata na ambao ulisababisha kuzuka ghasia nchini humo.

Maelezo ya picha,

Zaidi ya wakimbizi 30,000 wanaoishi Tanzania warudi kwao Burundi

Kwa miongo kadhaa Tanzania imefungua mipaka yake kwa maelfu ya watu wanaokimbia ghasia nchini mwao hasa nchini Burundi, Rwanda na Jamhuri ya Demokrasi ya Congo.

Wakosoaji wa mpango huo wanadai kuwa serikali za Tanzanian na Burundi zinatumia mpango huu kujaribu kuifanya jamii ya kimataifa kuamini kuwa amani imerejea Burundi, licha ya makundi mengine ya kutetea haki yakisema kuwa ukiukaji wa haki za binadamu nchini humo bado unaendelea.

Maelezo ya picha,

Zaidi ya wakimbizi 30,000 wanaoishi Tanzania warudi kwao Burundi

Shirika la kuwahudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa - UNHCR -linaunga mkono, lakini haliwashauri wakimbizi hao kurudi nyumbani.

Baadhi wanasema kuwa sio kuwa wanarudi nyumbani kwa sababu wana uhakika asilimia mia moja kuwa nchi yao iko salama, bali wanarudi kwa kile wanajua kuwa ni chao na walichokijua kwa miaka mingi ya maisha yao.