Kampuni ya magari Aston Martin kuzindua gari linalopaa angani

Kampuni ya kutengeneza magari ya fahari, Aston Martin imezindua mipango mipya ya kuunda gari linalopaa liitwalo "sports car for the skies". Ikishirikiana na Rolls Royce na wahandisi wa chuo kikuu Cranfield wanapanga kuzindua magari yatakayopaa kama ndege miaka miwili ijayo. Je, unadhani watu watakuwa wanapaa na magari hewani katika siku za usoni? Tupe maoni yako kwenye ukurasa wetu wa Facebook, bbcnewwsSwahili.