Kwa Picha: Poda ya asili ya wasichana na wanawake wa Kiislamu wa jamii ya Rohingya nchini Bangladesh

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Mkimbizi wa Rohingya Laila Begun,mwenye miaka 23, akiwa amepaka poda iitwayo thanaka katika kambi ya Balukhali nchini Bangladesh

Mpiga picha wa Reuters Clodagh Kilcoyne ametengeneza mfululizo wa picha za waislamu wa Rohingya wasichana na wanawake katika kambi mbalimbali za kusini mwa Bangladesh, akipata picha za urembo wao wa asili


Msichana mkimbizi wa jamii ya Rohingya kwa jina Rufia Begun mwenye umri wa miaka 9 akiwa ametulia kupata picha huku akiwa amepaka poda katika kambi ya Balukhali nchini Bangladesh Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Msichana mkimbizi wa jamii ya Rohingya kwa jina Rufia Begun mwenye umri wa miaka 9 akiwa ametulia kupata picha huku akiwa amepaka poda katika kambi ya Balukhali nchini Bangladesh

MKimbizi wa Rohingya Shamima, mwenye miaka 10, akiwa kwenye kambi ya Jamtoli Haki miliki ya picha Reuters
Image caption MKimbizi wa Rohingya Shamima, mwenye miaka 10, akiwa kwenye kambi ya Jamtoli

Zaidi ya watu wa jamii ya Rohingya 700,000 wamekimbia makwao na kukimbia kushtakiwa katika jimbo la Rakhine nchini Myanmar na kukimbilia nchini Bangladesh tangu mwezi Agosti mwaka 2017.

Idadi ya warohingya wanaokaribia milioni moja nchini Myanmar ni moja kati ya jamii ya watu wachache waishio nchini humo.

Jeshi la Myanmar limesema linapambana na wanamgambo wa Rohingya wakikana kuwalenga raia.

Mkimbizi wa Rohingya Laila Begun,mwenye miaka 23, akiwa amepaka poda iitwayo thanaka katika kambi ya Balukhali nchini Bangladesh Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Mkimbizi wa Rohingya Laila Begun,mwenye miaka 23, akiwa amepaka poda iitwayo thanaka katika kambi ya Balukhali nchini Bangladesh

Picha za wasichana waislamu wa Rohingya na wanawake kwenye kambi za Cox Bazaar, mji ukio kusini mwa pwani ya mashariki mwa Bangladesh zilipigwa na Kilcoyne.

Mkimbizi Senuara Begun, miaka 14 akiwaamejipaka rojo la thanaka katika kambi ya Jamtoli Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Mkimbizi Senuara Begun, miaka 14 akiwaamejipaka rojo la thanaka katika kambi ya Jamtoli
Mkimbizi wa Rohingya, Romzida, miaka 8 akiwa kwenye kambi ya Shamlapur Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Mkimbizi wa Rohingya, Romzida, miaka 8 akiwa kwenye kambi ya Shamlapur

Poda hii iliyo mithili ya tope pia husaidia kuzuia miale mikali ya jua, kuifanya ngozi kupoa.

Mkimbizi wa Rohingya Zinu Ara Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Mkimbizi wa Rohingya Zinu Ara

Poda hii ya manjano hukauka na kuwa kavu usoni, huzuia pia kuumwa na wadudu.

Rohingya refugee Nur Kayas, aged 6, poses for a photograph as she wears thanaka paste at Kutupalong camp in Cox's Bazaar, Bangladesh Haki miliki ya picha Reuters

Poda hii, imekuwa ni kawaida miongoni mwa jamii ya wasichana na wanawake wa kiislamu jamii ya Rohingya.

Mtoto Sufaida mwenye miaka 7 akiwa katika kambi ya Kutupalong Cox Bazaar, Bangladesh Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Mtoto Sufaida mwenye miaka 7 akiwa katika kambi ya Kutupalong Cox Bazaar, Bangladesh

Juhara Begum mwenye miaka 13 hapo chini anamwambia Kilcoyne kuwa'' ninapenda sana kujiremba, ni utamaduni wetu''.

''Jeshi lilifyatua risasi na kutuchinja.Niliishi milimani, ambako kuna joto kutokana na jua kali''.

Rohingya refugee Juhara Begum, aged 13, poses for a photograph as she wears thanaka paste at Jamtoli camp in Cox's Bazaar, Bangladesh Haki miliki ya picha Reuters

Begun aliwasili Cox's Bazar mwezi Septemba mwaka jana baada ya kukmbia mashambulizi ya kijeshi katika kijiji chake kilicho katika jimbo la Rakhine.

Alilazimika kutembea kwa siku tano kufikia eneo la mpaka lililo salama na kambi iliyokuwa na watu wengi ya Jamtoli.

''Ninaweza kuishi bila kula wali lakini si bila poda'', alisema Begum.

Mkimbizi wa Rohingya Toyuba, 18 kutoka kambi ya Kutupalong Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Mkimbizi wa Rohingya Toyuba, 18 kutoka kambi ya Kutupalong

Zannat Ara, mwenye miaka tisa kutoka kambi ya wakimbizi ya Kutupalong alisema: ''Ninapaka poda kuuweka uso wangu kuwa safi na kuna wadudu wanauma usoni lakini poda hii huwafukuza''.

Zannat Ara, ana miaka 9 katika kambi ya Kutupalong Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Zannat Ara, ana miaka 9 katika kambi ya Kutupalong

Msichana kutoka jamii ya Rohingya akiwa katika kambi ya Shamlapur Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Msichana kutoka jamii ya Rohingya akiwa katika kambi ya Shamlapur

Picha na Clodagh Kilcoyne.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii