Ni kwa nini Mombasa Kenya inageuka samawati?

Soko la Mackinon Mombasa
Image caption Soko la Mackinon mjini Mombasa Kenya

Uamuzi wa kaunti ya Mombasa kuamuru wamiliki wa majumba yote katikati mwa mji huo yapakwe rangi ya samawati na nyeupe umezua hisia tofauti huku baadhi ya wakaazi wakifurahia mabadiliko hayo na wengine hasa wafanya biashara wakilalamika.

Miongoni mwa wafanya biashara waliowasilisha kesi mahakamani wakipinga uamuzi huo lakini hawakufanikiwa.

Wameishutumu vikali serikali ya kaunti hiyo chini ya uongozi wa Gavana Hassan Joho kuwashurutisha kupaka rangi ambayo haiwapendezi.

``Tumefuata sheria ya kaunti lakini hatujafurahishwa na uamuzi huo,'' anasema Cynthia Luvanda ambaye ni mfanya biashara wa simu.

Haki miliki ya picha TONY KARUMBA
Image caption Gavana Hassan Joho amesema utawala wake umeidhinisha mpango huo kuhakikisha kuwa maeneo ya katikati mjini na mji mkongwe Mombasa yapakwa rangi sare

``Imebidi nikubali kwa sababu sina uwezo wa kukiuka sheria hiyo. Mimi ni muuzaji simu ningependa kijani kibichi inayoashiria Safaricom.''

Agizo la serikali ya kaunti linasemaje?

Hatua ya miji kupakwa rangi inatokana na ilani iliyotolewa na serikali ya kaunti kwa wakaazi na wamiliki wa majengo mnamo Machi mwaka huu 2018.

Agizo hilo linasema majengo yanastahili kupakwa ranginyeupe na samawatiinayoachiria bahari ya Hindi.

Utawala wa kaunti ulitoa siku 14 kutiii agizo la kutayarisha upakaji rangi na siku 30 kutoka siku ya kuanza kutekelezwa ka agizo hilo kukamilisha shughuli hiyo.

Agizo hilo lilipitishwa baada ya vikao na na wakaazi wa mji huo katika baraza la wazi kuhusu utekelezaji wa mpango huo, ambapo hisia inayotajwa kuibuka ni kwamba ingekuwa njia ya rahisi ya kurudisha urembo na hadhi ya mji huo mkongwe na wa pili kwa ukubwa Kenya.

Wanawake wachimba makaburi nchini Cameroon

Gavana wa Mombasa ahojiwa na polisi Kenya

Gavana wa Mombasa, Hassan Ali Joho amesema utawala wake umeidhinisha mpango huo utakaohakikisha kuwa maeneo ya katikati mjini na mji mkongwe Mombasa kupakwa rangi sare.

Hassan Noor ni muuzaji wa nguo za watoto, na kwa miaka yote hiyo rangi ya biashara yake imekua ni ya manjano lakini sasa amelazimika kubadilisha rangi hiyo na kupaka samawati na nyeupe.

``Sasa ni vigumu kumuelekeza mteja mpya kwangu kwa sababu majumba yote yamefanana. Tumeshangaa sana maanake hatujakataa kupaka rangi zetu za biashara. Nakubali mji unang'ara lakini haupendezi kila jumba likiwa na rangi sawa.''

Baadhi ya wakaazi wamepongeza kaunti ya Mombasa kwa mabadiliko hayo, wakisema Mombasa sasa ina sura mpya na inang'aara hata usiku kwani serikali ya kaunti ya Mombasa imeamuru wafanya biashara wahakikishe kuna mwangaza wa kutosha usiku.

Image caption Waziri wa uchukuzi na miundo mbinu katika kaunti ya Mombasa Tawfiq Balala

Waziri wa uchukuzi na miundo mbinu Tawfiq Balala anaeleza sababu yao ya kuchukua uamuzi huo, 'Mombasa katika hii miaka iliyopita imekua chafu sana ndio kwa maana tukaamua kurejesha ile hali ya zamani ya Mombasa.

'Kama mjuavyo Mombasa ilikua inavutia watalii wengi ambao kwa sasa wamepungua. Rangi ya samawati ni ya bahari, maji ndio rasilimali yetu kubwa na yana rangi mbili ya samawati na nyeupe.

Watu wengi wamefurahia hata ukiangalia kwenye mitandao ya kijamii wamesifu kaunti ya Mombasa. Lakini sio rahisi kufurahisha kila mtu ndio kwa maana wengine wao wanalalamika.''

Kwa wauzaji na wapaka rangi ni msimu wa kuvuna.

Ukiwa Mombasa utawaona wapaka rangi juu ya majumba wakiwa kazini furaha tele.

Dan Bonyo anasifu kaunti ya Mombasa kwa mradi huu.

`Kusema kweli tumeangukia, na kila siku si Jumapili lakini kwa sasa nitasema mambo mazuri kwetu, kazi ni nyingi ingawaje malipo si ya juu sana kwa sababu tuko wengi na kuna wengine wameingilia kazi hii lakini ni wapakaji rangi bandia hawana ujuzi' anasema Bonyo.

Kutoka hapa tungetaka Joho aanze kuusafisha mji ambao una taka nyingi zinazoipatia kaunti yake sura mbaya.''

Kadhalika wakaazi na wamiliki wa majengo Mombasa wametakiwa kusafisha njia wanazotumia watu kutembea mitaani katika maeneo wanayoishi.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii