Wema Sepetu: Apigwa faini ya shilingi milioni mbili za Kitanzania kwa kesi ya umiliki wa bangi iliyomkabili

Wema Sepetu

Mahakama ya kisutu mjini Dar es Salaam imempata na hatia mshindi wa malkia wa Urembo nchini humo mwaka 2006 Wema Sepetu na kumpiga faini ya shilingi milioni mbili za Kitanzania kufuatia kesi ya umiliki wa mihadarati iliokuwa ikimkabili.

Aidha mahakama hiyo imesema kuwa Wema atahudumia kifungo cha mwaka mmoja iwapo atashindwa kulipa faini hiyo.

Wema Sepetu ambaye alishinda taji la malkia wa urembo nchini humo 2006 atahukumiwa pamoja na washtakiwa wengine wawili Angelina Msigwa na Matrida Seleman Abas .

Hakimu mkaazi Thomas Simba aliambia mahakama hiyo siku ya Jumatatu kwamba hukumu hiyo iliotarajiwa kutolewa siku ya Jumatatu sasa itatolewa Ijumaa baada ya kukamilika kwa maswala machache yaliokuwa yamesalia.

Inadaiwa kwamba mnamo tarehe 4 mwezi Februari mwaka uliopoita , Wema na wenzake walipatikana wakimiliki misokoto ya bangi katika eneo la Kunduchi Ununio.

Wema pia ameshtakiwa kwa kuvuta bangi .

Mwaka uliopita, maafisa wa polisi nchini Tanzania walianzisha msako dhidi ya watu maarufu baada ya baadhi yao kuhusishwa na ulanguzi wa mihadarati.

Mapema, mwanasheria mkuu Costantine Kakula, alisema kuwa kesi hiyo iliwasilishwa mbele ili hukumu hiyo itolewe na kwamba upande wa mashtaka ulikuwa tayari kusikiliza hukumu hiyo.

Kesi hiyo ilifikia awamu ya kutolewa kwa hukumu hiyo baada ya mawakili wa walalamishi , Albert Msando na mwenzake wa upande wa mashtaka Constantine Kukula kuwasilisha hoja zao za kwa nini washtakiwa hao wanapaswa kupatikana na hatia au la.

Ilidaiwa kwamba mnamo tarehe 6 mwezi Februari, vitu hivyo vilivyopatikana kutoka kwa washukiwa hao vilipelekwa kwa mwanakemia mkuu wa serikali kwa uchunguzi na kuthibitishwa kwamba ushahidi huo ulikuwa gramu 1.08 za bangi.

Tarehe 8 Februari, washukiwa walipelekwa tena kwa mwanakemia wa serikali ili kufanyiwa vipimo vya mkojo ambapo baada ya kuchunguzwa ilibainika kwamba ilikuwa na bangi.

Hatahivyo upande wa malalamishi ulipinga matokeo hayo ukisema kuwa yeye hupokea wageni wengi nyumbani kutokana na umaarufu wake.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii