Mashine kubwa zinazoisaidia China kuunganisha ulimwengu

Wakati china ikitekeleza moja kati ya miradi mikubwa ya miundo mbinu, mradi mkubwa katika historia, pia unabadili pia namna ambavyo reli zinatengenezwa

Mradi huu wa shauku kubwa wa rais Xi jinping, ulianzishwa mwaka 2013, ukiwa na lengo la kuunganisha theluthi mbili ya watu walio katika nchi 70 duniani kupitia mtandao wa njia ya ardhi na bahari.

Maafisa wanaongelea kuhusu uwekezaji wenye kugharimu trilioni za dola, kutoka kwenye mabenki, nchi washirika na serikali ya China.

Wakati malengo yanaweza kuonekana kama vile yasiweze kufikiwa,sehemu ya uwekezaji tayari unaonekana nchini China na je ambapo mashine mbalimbali mpya zimekuwa zikijenga mradi wa Ardhi na barabara (BRI) kwa kasi ya hali ya juu.

Mradi huo hata hivyo una utata. Wakosoaji wanasema unayaacha mataifa ya Afrika na mzigo mkubwa wa madeni ya mabilioni ya dola watakazokuwa wanadaiwa na China. Wanapuuzilia mbali miradi hiyo kama sehemu ya sera ya mambo ya nje ya China ya kueneza udhibiti wao.

Hata hivyo, ushahidi wa Mkanda huu na Barabara tayari unaonekana China na kwingineko, ambapo mashine kubwa zinajenga reli kwa kasi ajabu.

Ujenzi wa Madaraja

Unawezaje kujenga reli za mwendo wa kasi kwa haraka ambapo sehemu kubwa ya njia zake lazima zipite zikivuka mabonde ili kuepuka kupinda?

Mashine ya kujenga madaraja ziitwazo kwa jina la utani ''Shetani mkubwa'' ni mashine inayofanya kazi mbalimbali kama vile kubeba, kunyanyua na kupanga vyuma vya reli.

Baada ya kulaza vyuma vya reli kwa, chombo chenye ukubwa wa mita 92 kikisaidiwa na matairi 64-inashindilia sehemu ambayo vyuma vya reli vimelazwa

Hata chombo hicho kikiwa na mzigo mkubwa kuna uwezo wa kutembea mpaka umbali wa kilometa 5 kwa saa, kuhakikisha kuwa mchakato huu unakwenda kwa kasi kuliko njia za kizamani ambazo zilihitaji mashine nyingi zaidi.

Zimesaidia sana katika miradi ya reli, ikiwemo zile zinazounganisha China na Mongolia na kuifanya kufikia malengo ya kuwa na reli ya mwendo kasi ya umbali wa kilomita 30,000 kufikia mwaka 2020.

Barabara ya chini ya ardhi

Kuelekea kusini, ujenzi wa mradi wa njia ya Su'ai mjini shantou , si mbali na Hong Kong,umewezesha kufanikisha uchimbaji wa barabara ya chini ya njia sita urefu wa kilomita tano

Wakati barabara ya chini ya ardhi itakapofunguliwa mwaka 2019,maafisa wana matumaini kuwa wataboresha miundo mbinu ya usafirishaji ya shantou kwa wakati ili iwe moja kati ya maeneo muhimu 15 yanayoungana na bandari.

Wajerumani walikuwa wakiongoza kwenye utaalamu huu wa kutengeneza mashine kwa ajili ya mradi wa chini ya ardhi.Lakini hivi karibuni, makampuni ya China yameanza kutumia teknolojia yao

Kama ilivyo kwa wenzao wa Ujerumani, China ina kifaa mithiri ya sahani yenye uwezo wa kukata ardhini na kwenye miamba

Ikiwa na uzito wa tani 4,000.Vifusi vinavyotokana na kukatwa kwa ardhi na miamba hukusanywa na kutolewa nje ya handaki

Ujenzi wa Reli

Wakati wa mradhi huo ukiendelezwa nchini China, miradi migine iliyofadhiliwa na China imekuwa ikiendelea maelfu ya maili katika nchi nyingine.

Reli ya Mombasa mpaka Nairobi nchini Kenya ilimalizika mwezi Mei mwaka 2017 na kuwa gumzo kimataifa na kukamilika kabla ya muda uliopangwa.

Reli hii yenye urefu wa kilomita 480 ni ya kwanza nchini Kenya tangu uhuru .

Ikiwa na ufadhili wa 90% kutoka China kupitia Exim Bank ya nchini humo, ni reli ya kwanza nje ya China iliyojengwa kwa kutumia mashine za China.

Kuelewa jinsi reli ilivyojengwa kwa kasi ya umbali wa mita 700 kwa siku, tazama mashine zilizotumika kutandika vyuma vya reli.

Ili ziweze kufanya kazi kikamilifu, mashine hizi bado zinahitaji nguvu kubwa ya watu kufanya kazi

Wafanyakazi na wahandisi wa China wanahangaika kuunda vijisehemu vya njia ya reli

Wanapaswa kuhakikisha kuwa sehemu za njia ya reli ziko katika mahali pake sahihi kwa vipimo vyake maalum

kumekuwa na masuala yaliyoibuliwa kuhusu usalama wao.Mwaka jana Mhandisi wa China aliyekuwa akijenga reli ya Mombasa-Nairobi aliliambia shirika lahabari la China kuwa wakiwa kazini ajali ni jambo la kawaida

''Zinapotokea, mara zote huwa ni mbaya sana'' .Mradi wa reli kwa sasa umeendelea kuwa maarufu katika nchi za Afrika na umejipanga kufanyika mabadiliko

Reli ya Nairobi-Mombasa inachukua nafasi ya ile ya zamani tangu kipindi cha ukoloni iliyokuwa ikichukua saa kumi tofauti na mpya ambapo watu wanasafiri kwa saa nne.Na zaidi ya abiria 870,000 wamesafiri kwa njia hiyo.

Wakati huo huo kazi imeendelea kufanyika kupanua njia kwenda maeneo ya kisumu,kwa mkopo wa dola bilioni 1.5 kutoka benki ya Exim ya China, hatimaye itaweza kuunganisha Uganda,Rwanda, Sudani Kusini na Ethiopia.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii