Wanajeshi wa Israel waliokoa kundi la White Helmets kutoka Syria

Members of the White Helmets in Aleppo, June 2014 Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Wanachama wa kundsi la White wakiokoa huko Aleppo kaskazini mwa Syria

Israel imesema imeendesha oparesheni ya kuliokoa kundi linalofahamika kama White Helmets civil defence group, kutoka eneo la vita kusini magharibi mwa Syria.

Karibu watu wa kujitolea 422 na familia zoa walipelekwa nchini Jordan kupitia eneo linalokaliwa na Israel la Golan Heights.

Uingereza, moja ya nchi zinazoiomba Israel kuchukua hatua hiyo imeipongeza na kusema itasaidia kuwatafutia makao watu hao.

The White Helmets wanajitaja kama watu wa kujitolea ambao husaidia watu kutoka sehemu zinazokumbw na vita nchini Syria.

Wafuasi wa rais wa Syria Bashar al-Assad na washirika wake wa Urusi, wanasema the White Helmets wanawaunga mkono waasi na pia kuwa wana uhusiano na makundi ya kijihad.

Kwa nini oparesheni hiyo ikafanyika?

Vikosi vya ulinzi vya Israel IDF vinasema vilichukua hatua hiyo kufuataia ombi kutoka Marekani, Uingereza na mataiafa ya Ulaya.

White Helemets walikuwa wamekwama eneo lililo kusini magharibi mwa Syria, karibu na mpaka na eneo la Golan Heights baada ya harakati iliyochukuliwa na jeshi la Syria.

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Waasi wa syria huko Quneitra walifanya uharibifu kabla ya kuondoka

Harakati hizo zilianza Juni na zimeshuhudia kuafikiwa kwa makubaliano kadhaa ambayo yamechangia kuhamishwa kwa vikosi vya waasi kutoka maeneo ya Deraa na Quneitra kwenda sehemu zilizo mbali kaskazini.

The White Helmets uhudumu maeneo ya waasi licha ya wao kusema kuwa hawana upendeleo.

Waliookolewa walisafirihswa kwenda kwa mpaka wa Golan Heights na kupelekwa na vikosi vya Israel kwenda Jordan.

Mpango ho ulikuwa na kuwaokoa wahudumu 800 wa White Helmets lakinini ni watu 422 walifanikiwa kuokolewa.

Image caption Golan Heights

Mada zinazohusiana