Mnangagwa: Siwezi kuwanyang'anya wakulima wa kizungu mashamba yao

Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa

Rais wa Zimbabewe Emmerson Mnangagwa amewaambia wakulima wa asili ya kizungu kuwa ardhi zao hazitachukuliwa

Kauli hii imekuja wakati taifa hilo likielekea kwenye uchaguzi mkuu.

Serikali ya aliyekuwa Rais wa nchi hiyo Robert Mugabe ,ilikuwa inaunga mkono kunyang'anywa kwa mamia ya mashamba ya wazungu ambayo waliona kuwa yalikuwa yanachukuliwa bila haki.

Mnangagwa ameuambia Umma mjini Harare kuwa sera hiyo ya kukanganya ni kitu kilichopita.

''Tunapaswa kuacha uzungumza kuhusu nani anamiliki shamba kwa kutazama rangi''.Alieleza.

''Ni uhalifu kuzungumza namna hiyo, Mkulima, mkulima mweusi, mkulima wa kizungu, wote ni wakulima wa Zimbabwe.''

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Chamisa ni maarufu miongoni mwa vijana

Hatua ya Rais Mnangagwa kushughulikia malalamiko ya wapiga kura wenye asili ya wazungu imekuja wakati ambapo kunatarajiwa kufanyika uchaguzi wa kihistoria tarehe 30 mwezi Julai.

Utakuwa uchaguzi wa kwanza wa urais tangu Mugabe alipoondolewa madarakani mwezi Novemba, na kumaliza utawala wake uliodumu kwa miaka 37.

Raia wa Zimbabwe wenye asili ya weupe wamekuwa wakipigia kura vyama vya upinzani kama vile Movement for Democratic Change(MDC).

Rais huyo amesema kuwa serikali yake si ya kibaguzi na ameeleza jinsi mtangulizi wake alivyoshindwa kwenye suala ya mabadiliko ya sera za umiliki ardhi.

kukamatwa kwa ardhi inayomilikiwa na wazungu kulisababisha kilimo kudorora na kuondoka kwa wakulima hao , pia ukosefu mkubwa wa ajira kulikowaathiri wafanyakazi wa mashambani wenye asili ya weusi.

Kuna zaidi ya vyama vya siasa 120 vilivyosajiliwa wakati huu wa uchaguzi, na huenda kutakuwa na wagomea 23 wa urais.

Rais huyo anapewa nafasi kubwa kushinda, lakini wachambuzi wa mambo wanasema ana maadui pia kwa pande zote mbili, kutokana na kumuangusha Mugabe.

Kiongozi wa chama cha upinzani ,Nelson Chamisa, ambaye alikuwa maarufu zaidi mwezi Februari ndani ya chama cha MDC.

Ni kipenzi cha vijana na wasio na ajira, atakuwa rais mdogo wa umri ambaye hajawahi kutokea nchini humo

Mada zinazohusiana