Nyaraka kuhusu mahusiano kati ya msaidizi wa Trump na Urusi zatolewa

Carter Page amekuwa akishutumiwa kuwa na mahusiano na maafisa wa intelijensia nchini Urusi Haki miliki ya picha EPA
Image caption Carter Page amekuwa akishutumiwa kuwa na mahusiano na maafisa wa intelijensia nchini Urusi

Shirika la upelelezi nchini Marekani liliamini kuwa msaidizi wa Donald Trump kwenye masuala ya sera za mambo ya nje Carter Page ''alikuwa akishirikiana na serikali ya Urusi '' wakati wa kampeni za uchaguzi wa mwaka 2016, hii ni kwa mujibu wa nyaraka mpya zilizotolewa.

Page amekuwa akikana shutuma hizo

Rais wa Marekani amesema kuwa inaonyesha kuwa kampeni yae ilikuwa inaingiliwa na majasusi

maombi ya kufanyika upepelezi yalikubalika baada ya majaji kadhaa kukaa kwenye mahakama ya upelelezi kuhusu inteijensia ya nje.

Kwa mujibu wa nyaraka, ''FBI wanaamini kuwa jitihada za Urusi zilikuwa zikiratibiwa na Page na labda watu wengine waliokuwa wakiambatana kwenye kampeni za Trump.

Nyaraka zinasema kuwa Page ''alianzisha mahusiao na maafisa wa serikali ya Urusi, wakiwemo maafisa wa intelijensia''.

Carter Page ni nani?

Bwana Page ni mshauri wa masuala ya nishati akiwa na uhusiano wa muda mrefu na Urusi.

Mwezi Machi mwaka 2016, Trump alimtamgua Page kuwa msaada mkubwa katika kushauri masuala yahusuyo sera za mambo ya nje kwenye kampeni zake.

Hata hivyo, baada ya shutuma dhidi yake kujitokeza, Bwana Page alijiuzulu wadhifa wake.

Page amekana shutuma zote dhidi yake.

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Bwana Page alifanya kazi na Rais wa Marekani Donald Trump kwenye Kampeni za mwaka 2016

Nyaraka hizo zimetolewa siku tisa baada ya Raia wa Urusi 12 waliposhtakiwa kudukua maafisa wa Marekani kwenye uchaguzi wa Marekani

mpaka sasa, watu 32 wameshtakiwa , wengi wao raia wa Urusi ambao hawakuwepo wakati wa mashtaka sambamba na makampuni matatu na washauri wa zamani wa Trump.

Siku chache baadae, Trump alikutana na Rais wa Urusi, Vladmir Putin, mjini Helsinki na aliulizwa na wana habari kama anaamini kuwa Urusi iliingilia uchaguzi wa mwaka 2016.

''Rais wa Urusi anasema si Urusi.Sioni sababu kwa nini iwe Urusi'', alijibu ikionekana kuwa aliiunga mkono Urusi dhidi ya taasisi zake.

Trump ajichanganya na kauli yake kuhusu Urusi

Trump shutumani kwa kuitetea Urusi

Rais Trump amualika Putin Washington

Siku iliyofuata baada ya watu kuonyesha ghadhabu zo kuhusu kauli yake, alisoma taarifa yake aliyoiandaa akisema kuwa alimaanisha ''sioni sababu isiwe Urusi''

Siku ya Alhamisi Ikulu ya Marekani ilitangaza kuwa ilimualika Putin mjini Washington mwezi Oktoba-tangazo ambalo lilimshtua mkurugenzi wa idara ya intelijensia Dan Coats.

Bwana Coats, aliyekuwa akizungumza kwenye mkutano wa masuala ya usalama mjini Colorado alionekana kwenye picha ya video akicheka, kabla ya kusema ''tukio hilo litakuwa la kipekee''.

Lakini alijitetea kuwa kauli yake haikumaanisha kumvunjia heshima au kumkosoa Rais Trump.