Picha ya mtoto akilala kwenye reli ambayo imezua maoni nchini Uingereza

Incident at Trowbridge railway station on Saturday afternoon Haki miliki ya picha Tim Brown
Image caption Tim Brown, ambaye alichukua picha hiyo ametaja tukio hilo kuwa lisilo la kuaminika.

Picha ya mtoto ambaye alionekana akilala chini huku kichwa chake kikikaribiana na reli imezua maoni mengi na kuchangia kuanzishwa uchunguzi kutoka kwa polisi wa uchukuzi nchini Uingereza.

Picha hiyo iliyochapishwa mitandao kuhusu kisa hicho kilichotokea eneo la Trowbriger, Wiltshire siku ya Jumamosi jioni imesambazwa pakupwa mitandaoni.

Tim Brown, ambaye alichukua picha hiyo ametaja tukio hilo kuwa lisilo la kuaminika.

Alisema kuwa wakati alimueleza mwanamme ambaye pia alikuwa na wasichana wawili kuwa watu hujeruhiwa na hata kuuliwa wakifanya hivyo, mwanamume huyo alijibu kuwa treni haijafika na kwamba mtoto alikuwa anaagalia tu reli.

Bw Brown anayefanya kazi na Network Rail anasema alimuambia kuwa wakati mwingine treni ambayo haikuwa kwennye ratiba inaweza kupita wakati wowote kisha akaripoti kisa hicho kwa mlinzi.

Polisi wa uchukuzi wa Uingereza walithibitisha kisa hicho na kusema kuwa walikuwa wanasubiri taarifa zaidi kabla ya kuanzisha uchunguzi.

Msemaji wa Great Western Railway (GWR), inayosimia kituo cha Trowbridge railway alisema: Wakati mwingine treni hupita kwenye kituo bila kusimama au bila ya kuonekana kwenye ratiba ikipita kwa mwendo wa kasi.

Mada zinazohusiana