Karume: Tutaendelea kuikosoa serikali Tanzania
Huwezi kusikiliza tena

Fatuma Karume: Tutaendelea kuikosoa serikali na kutetea haki Tanzania

Rais wa Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS) amesema wataendelea kuikosoa serikali kwa kuwa wanasheria wanatetea haki za watu.

Serikali ya Tanzania iliwahi kutishia kukifuta Chama hicho kwa madai kuwa kinajiingiza katika Siasa.

Mwandishi wetu Arnold Kayanda amezungumza na Rais wa TLS Bi Fatuma Karume aliyechukua mamlaka baada ya aliyekuwa Rais wa Chama hicho Tundu Lissu kushindwa kuendelea na uongozi kutokana na kupigwa Risasi na watu wasiofahamika.

Mada zinazohusiana