Mwanamke anayetumia mtandao wa Instagram kutoa ushauri kwa wanawake wanaodhulumiwa kimapenzi
Huwezi kusikiliza tena

Mwanamke anayetumia Instagram kuwashauri wanawake wanaodhulumiwa kimapenzi

Natasha Toffa anatumia mtandao wa Instagram kuwasaidia wanawake kote duniani wanaopitia unyanyasaji wa kinyumbani kwa kuwapa ushauri. Kwa mara ya kwanza mwanamke huyo ameenda kumtembelea mteja wake ili kumpatia ushauri nasaha zaidi.

Je, umeshuhudia watu kama Natasha wanaotoa usaidizi kwa wanawake nchini mwako?

Tuwasiliane kwenye Facebook bBBCSwahili.com