Densi inayowasaidia walemavu kukabiliana na unyanyapaa
Huwezi kusikiliza tena

Densi inayowasaidia walemavu kukabiliana na unyanyapaa Kenya

Watu walemavu hukumbwa na changamoto sio haba, na mara nyingi hukosa vitu muhimu sana kama elimu, na hata wakati mwingine nafasi za ajira. Wale wanaoishi katika nchi ambazo hazijaendelea na hasa katika jamii ambazo walemavu huonekana kama watu waliolaaniwa huwa na changamoto nyingi zaidi. Lakini wengi wameweza kustahimili haya yote na kuibuka vielelezo katika jamii. Nchini Kenya kikundi cha dance into space ambacho wahusika wengi ni walemavu kinatumia densi kupambana na unyanyapaa. Mpiga picha wetu Hassan Lali alikutana na kundi hilo katika eneo la Siaya Magharibi mwa Kenya.

Mada zinazohusiana