LHRC waunga mkono Marekani kuingilia demokrasia Tanzania

LHRC
Image caption Mkurugenzi wa LHRC Anna Henga, (katikati) hali ya haki za binadamu nchini humo kwa miaka ya hivi karibuni imekuwa ikiporomoka

Kituo cha sheria na haki za binadamu nchini Tanzania kimeunga mkono maombi ya Seneta wa New Jersey, Bob Menendez kwa raisi Donald Trump kuteua balozi wa Taifa hilo nchini Tanzania ili kufanya jitihada za kushughulikia kupinga ukiukwaji na uvunjaji wa demokrasia nchini akidai hali ilivo hivi sasa ni ya kuhofia.

Akiongea na waandishi wa habari mkurugenzi wa kituo hicho Anna Henga, amesema hali ya haki za binadamu nchini humo kwa miaka ya hivi karibuni imekuwa ikiporomoka siku hadi siku na kutokana na baadhi ya viongozi kutumia vibaya madaraka yao ama kwa maslahi yao binafsi ama kuzifurahisha mamlaka za juu yao.

Nyoka na 'Bundi wa miujiza', marufuku katika uchaguzi Zimbabwe

Trump aionya Iran 'isiijaribu Marekani'

Bob Menendez ambaye ni wa chama cha Democratic nchini Marekani alitoa shinikizo kwa serikali ya Marekani kuteua mara moja mjumbe nchini Tanzania atakayeongoza jitihada za kidiplomasia zitakazosaidia kudidimiza kile alichokitaja kuwa 'mkondo wa hatua zisizo za kidemokrasia', kwa mujibu wa gazeti la The Citizen.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Bob Menendez ambaye ni wa chama cha Democratic nchini Marekani

Katika taarifa mpya ya kituo hicho kuhusu ukiukwaji wa haki za kiraia na kisiasa, kama ilivyo elekezwa katika mkataba wa kimataifa wa Haki za kiraia na Kisiasa wa mwaka 1996, na katiba ya Jamuhuri ya muungano wa Tanzania ya mwaka 1997 - kituo hicho kinasema kimekuwa kikifuatilia mwenendo wa uchaguzi mdogo wa madiwani katika kata 77.

Tanzania: Mbwa mpekuzi 'Hobby' yuko wapi?

Bi Henga ameeleza kuwa wamebaini ukiukwaji mkubwa wa haki za kibinadamu na kisiasa ikiwemo baadhi ya wagombea kuenguliwa katika kinyanganyiro hicho kwa sababu zisizo za msingi ikiwemo kiwango cha elimu na hata mgombea mmoja kushindwa kusoma neno 'Zinjanthropus'.

LHRC kinasema kimeshtushwa na mfululizo wa vitendo na kauli zinazotolewa na viongozi wa serikali zinazo kiuka katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania (1977) ikiwemo ile ya Waziri wa Mambo ya Ndani Kangi Lugola aliyoitoa Julai 21 2018 akielekeza askari wa usalama barabarani kutomfikisha mahakamani kwa kosa la kusababisha ajali kutokana na ubovu wa gari - bila kumlaza mtu huyo mahabusu.

Kufuatia hali hii kituo hicho kimeitaka tume ya taifa ya uchaguzi kuzingatia misingi ya sheria na kidemokrasia katika kusimamia uchaguzi sambamba na kuwa taka wananchi nao kutii na kuheshimu sheria na haki za binaadamu.

Mnangagwa: Siwezi kuwanyang'anya wakulima wa kizungu mashamba yao

LHRC limeahidi kuwasilisha kesi mahakamani dhidi ya watu au taasisi zinazokiuka haki za binaadamu.

Huwezi kusikiliza tena
Densi inayowasaidia walemavu kukabiliana na unyanyapaa Kenya

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii